Friday 29 October 2010

Swali: Jinsi gani ya kulainisha nyama ya ngombe?

Hongera Mama ntilie kwa kujaliwa kupata mtoto na nakutakia kila laheri katika malezi yake. Mimi nilikuwa na swali moja na ningependa wewe na pamoja ya wadua wa globu hii wachangie mawazo yao.

Nikipikaga pilau langu la nyama, mumu wangu anakuwaga anasema nyama ngumu, nimejitahidi kuongeza muda wa kuichemsha lakini bado naambiwa nyama ngumu kidogo. Sasa ningependa kuuliza njia gani niitumie ili kuilanisha nyama, nilishawi kutumia mapapai lakini sikupata matokeo makubwa sijui sikuyaweka muda mrefu au yalikuwa yameiva sana.

Nitashukuru mchango wenu.


Mama Shija

4 comments:

  1. Asante sana Mama Shija.Kuhusu nyama kuwa laini,mimi nyama huwaga naichemshia na tangawizi,limao, kitunguu saumu na chumvi kwa muda wa nusu saa. ikitoka hapo inakuwa laini.
    pia unaweza kujaribu kuimarinate na tangawizi kwa usiku mzima kisha ukaja ipika kesho yake.Kama hizo njia zote zikifeli na suggest utumie pressure cooker kwani hiyo ni mwisho wa matatizo yote ktk kushemshia vitu vigumu.

    ReplyDelete
  2. Mimi ninanuaga nyama ya ng'ombe au mbuzi wachanga, nilaini wala hauitaji kupoteza muda na mkaa au umeme kuchemsha muda mrefu. Jaribu hivyo alafu tueleze matokeo.

    ReplyDelete
  3. Hujatuambia baada ya kuichemsha, wakati wa kupika pilau huwa unaaikaanga nyama na viungo? maana hapo katika kuipika pilau ukiikaanga lazima itakuwa ngumu.

    Mtindi nao unalainisha sana nyama.

    ReplyDelete
  4. Anonymous 26 January 2011 01:58, unaonekana sio mfuatiliaji wa blog hii na huna ustaarabu. Ungekuwa mfuatiliaji mzuri ungejua kuwa alituomba samahani kwa kuwa yuko kwenye likizo ya uzazi. Get busy...!

    ReplyDelete