Tuesday 1 February 2011

NIMERUDI TENA

Hi
Wapenzi wa blog ya mapishi matamu, nimerudi tena baada ya likizo ndefu kidogo.Samahani kwa kuwa kimya mizunguko ya kimaisha ilinitinga kidogo na kama mnavyojua tena kuwa mama kwa mara ya kwanza unakuwa unamengi ya kujifunza kuhusu ulezi.Natumai kwa waliokuwa wazazi/ walezi mtakuwa mnanielewa kuhusu hilo.Anyway nimerudi ktk kuendeleza libeneke. Nitajitahidi kuwa na update kila mara nitakapokuwa naingia jikoni kukorofisha pishi jipya. Kama nilivyosema kipindi cha nyuma, kwa yeyote aliyekuwa na pishi lake na angependa ku-share nasi anakaribishwa kunitumia nami nitali-publish bila hiyana.
Asanteni kwa uvumilivu wenu.

Mama Ntilie

2 comments:

  1. Karibu tena maana tuliku-miss sana..

    Hongera kwa kupata mtoto na heri ya mwaka mpya.

    ReplyDelete
  2. Asante sana mdau Heri ya mwaka na wewe pia.Mi pia niliwamiss sana wadau sema majukumu yalinizidi ndo mana mkaona kimya kidogo.

    ReplyDelete