Monday, 20 September 2010

Mapishi ya Samaki wa kupaka


Mahitaji

  • Samaki (Tilapia 2)
  • Nyanya ya kopo (Tomato tin 1)
  • Kitunguu (Onion 1)
  • Tangawizi (ginger kiasi)
  • Kitunguu swaum (garlic clove )
  • Mafuta (Vegetable oil)
  • Pilipili (scotch bonnet pepper 1)
  • Tui la nazi zito (coconut milk 2 vikombe vya chai)
  • Curry powder 1/2 cha kijiko cha chai
  • Binzari nyembamba ya unga (ground cumin 1/2  kijiko cha chai
  • Binzari manjano (turmaric 1/2 kijiko cha chai
  • Chumvi (salt)
  • Limao (lemon 1)
  • Giligilani (fresh coriander)
Matayarisho
Marinate samaki na chumvi, limao, kitunguu swaum, tangawizi kwa muda wa masaa 6 au zaidi. Baada ya hapo wakaange au waoke katika oven mpaka waive ila usiwakaushe sana. Baada ya hapo saga pamoja nyanya ya kopo, kitunguu maji, kitunguu swaum na tangawizi. Kisha bandika huo mchanganyiko jikoni na upike mpaka ukauke maji kisha tia mafuta, binzari zote, curry powder, chumvi na pilipili na upike kwa muda wa dakika 5. Baada ya hapo tia maji kidogo (kama 1/2 kikombe) pamoja na tui la nazi. Acha uchemke mpaka tui liive na mchuzi ubakie kiasi. Baada ya hapo waweke samaki kwenye sufuria ya kuokea na kisha umwagie huo mchuzi juu ya hao samaki na owaoke (bake) kwa muda wa dakika 20. Ukisha toa kwenye oven katakata giligilani na utie kwenye hao samaki na hapo watakuwa tayari kwa kuliwa. unaweza kuwala na wali, ugali au chapati

7 comments:

  1. tunashukuru sana mpendwa kwa kutuelimisha kuhusu mapishi ya kitanzania. Mie nilikuwa na ombi moja toka kwako kuwa kama utaweza kutufunduha mapishi yafuatayo nitashukuru.
    1. Chapati
    2. Mkate wa kumimina
    3. Keki

    Maombi mengine nitaendele kuyaleta.

    Halafu kama itawezekana uwe unatuwekea na picha zinazoonyusha hatu kwa hatu unavyofanya mapishi yako mpaka unapokamilisha pishi lako.

    asante.

    Mariam wa Arusha.

    ReplyDelete
  2. mariam angalia old posts,mkate wa kumimina ndo mkate wa sinia,chapati katuonyesha ila sijaona keki

    ReplyDelete
  3. Mdau Mariam asante kwa kutembelea blog yangu. Kuhusu chapati na mkate wa kumimina(au wa sinia)angalia katika post zangu zilizopita (kama alivyosema mdau wa hapo juu) na kuhusu cake natumai kuja kuweka hapo mbeleni kwani kwa sasa nimebanwa kidogo na majukumu.

    Kuhusu kuweka picha hatua kwa hatua itakuwa ngumu kidogo maana siunajua tena ukiwa unapika unatakiwa uweke akili yote katika mapishi (namaanisha unahitaji ku-concetrate zaidi) ama sivyo unaweza kuunguuza au kusau kutia au kuzidisha chumvi na vitu kama hivyo.Ndiyo maana huwaga naona nimalize kupika kwanza ndo nipige picha.Ila nitajaribu kulifanyia kazi hilo swala.

    ReplyDelete
  4. Mama Ntilie,
    Ongela ombi langu kwenye list yako.
    Jinsi ya kuandaa mchuzi katika nyama/kuku etc. Shida ninayoipata ni kuwa mchuzi una'split, yaani unaona maji na mafuta hayachanganyiki kabisa hata unapojaribu kutumia unga wa kuongea mchuzi... sijui umenielewa.
    Wakati wa kupakua, unaona maji yana separate...

    ReplyDelete
  5. mamii wangu nashukuru kweli kwa hii blog yako kwani kwa mtu kama mie niliyehuku nje ya nchi nikiona maelezo ya kupika chakula cha bongo kweli nafarijika na kila siku lazima niingie kusoma vyakula...
    ombi langu ni moja, mie ni mwanafunzi ambaye nimekaa boarding school sana so mapishi yamenipita kabisa, na huwa najifunza kweli kupitia kwako hilo nakushukuru, ila kuna sehemu unakuwa unaniacha hasa ukiongela kuhusu kuweka kwenye oven so nilikuwa naomba ukiwaunaelezea kuhusu kuweka kwenye oven , na sie tunaotumia majiko ya kawaida(umeme, gas) tunafanyaje???
    naomba hapo uwe unatuambia kama inawezekana kutoweka kwenye oven basi tufanyaje.
    Thanks much!
    Shamila!

    ReplyDelete
  6. Kwa mdau wa mchuzi.
    Kuhusu mchuzi ku-separate hiyo inawezekana ikawa inasababishwa na kutokukadiria vitu sawa, ninamaana labda itakuwa unazidisha maji na mafuta nauku unakuwa unapunja nyanya.

    Kwa hiyo kama unahitaji mchuzi uwe mzito unatakiwa uvikadirie hivyo vitu (nyanya, mafuta na maji. Pia unaweza ukawa unatia viazi katika mchuzi wako hiyo pia husaidia mchuzi kuwa mzito.

    ReplyDelete
  7. Asante kwa kutuelimisha juu ya mapishi

    ReplyDelete