Monday 27 September 2010

Mapishi ya Bamia na chickpeas


Mahitaji

  • Bamia (okra 10)
  • Chick peas 1/2 kopo
  • Nyanya (fresh tomato 2)
  • Kitunguu (onion 1)
  • Kitunguu swaum (garlic paste 1/2 ya kijiko cha chai)
  • Curry powder 1/2 kijiko cha chai
  • Binzari manjano (turmaric 1/4 kijiko cha chai)
  • Mafuta (vegetable oil)
  • Chumvi ( salt)
  • Giligilani (fresh coriander)
Matayarishoa 
Andaa chickpeas kwa kuzitoa maganda, kisha osha bamia na uzikate katika vipande vya wastani. Baada ya hapo kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia kitunguu swaum, geuza geuza kwa muda wa dakika 3 kisha tia nyanya, curry powder, binzari manjano na chumvi na uzipike mpaka ziive. Baada ya hapo tia bamia na uzipike mpaka zikaribie kuiva kisha tia chickpeas. Zipike pamoja mpaka bamia ziive kisha malizia kwa kutia giligilani iliyokatwa na hapo mboga itakuwa tayari kwa kuliwa.Ni nzuri zaidi ikiliwa na wali.

(Msaada kwa anayejua jina la chickpeas kwa kiswahili)

Pishi hili nimejifunza kutoka kwenye kitabu kiitwacho (70 Traditional African recipes)

3 comments:

  1. Nimeishawahi kutoa coment hapa. Sina la ziada safari hii ila kukushukuru, huwa nasimama hapa kuangalia mapishi na wakati mwingine huwa naiga.
    Nimeona watu wanadai sana mapishi ya chapati, kwa nyongeza tu mapishi ya chapati ni rahisi na magumu, mara nyingi chapati hutoka ngumu, tueleze trick ya kuzifanya laini, je ni aina ya unga, joto la maji au nini? Asante sana kwa mcnango wako mkubwa, sasa hivi Watanzania wengi wana maisha kama ya nchi za kigeni, hususa nchi za ulaya, nadhani huu ni wakati mwafaka wa kuandika kitabu cha mapishi, utapata tu mchapaji ndugu yangu. Jaribu kutafuta sponsors ili ufaidike na ufundi wako. Nakutakia mafanikio katika hili pindi uamuapo. Nitakushangilia daima na kuwa mteja wako.

    ReplyDelete
  2. jina la chickpeas ni dengu kwa kiswahili na wengine wanaita njugu mawe kama sitakosea na pia zinajulikana kama garbanzo beans.

    ReplyDelete
  3. Asante sana mdau Anonymous no 1 kwa ushauri wako wa kutoa kitabu cha mapishi. Naahidi nitalifanyia kazi hilo swala muda muafaka utakapofika.

    Kuhusu chapati, Trick ya kuzifanya ziwe laini nazani nilishaelezea kwenye comment za chapati zilizopita ila kwa kukumbushia tu Kuhusu chapati kuwa laini inatokana na ukandaji na pia matumizi ya mafuta/siagi katika ukandaji. Labda jaribu, ukiwa unakanda unga badala ya kutumia siagi jaribu kukandia mafuta tu (vegetable oil) na ukisha kanda unga wa chapati uweke kwenye bakuli la plastic na uufunike kwa muda wa saa moja kabla yakuanza kuzikunja tena na mafuta. Nakisha kuzisukuma na kuanza kuchoma. Natumai hiyo inaweza kusaidia

    ReplyDelete