Thursday 16 September 2010

Mapishi ya Kachori


Mahitaji

  • Viazi mbatata (potato 4 vya wastani)
  • Nyama ya kusaga (mince beef 1 kikombe cha chai)
  • Kitunguu (onion 1 cha wastani)
  • Carrot 1
  • Hoho (green pepper 1/2)
  • Kitunguu swaum (garlic)
  • Tangawizi (ginger )
  • Binzari nyembamba (ground cumin 1/2 kijiko cha chai)
  • Binzari manjano (turmeric 1/2 kijiko cha chai)
  • Curry powder 1/2 kijiko cha chai
  • Limao (lemon 1/2)
  • Pilipili ya unga (chilli powder 1/2 kijiko cha chai)
  • Giligilani (coriander kiasi)
  • Chumvi (salt)
  • Mafuta (vegetable oil)
  • Unga wa ngano kiasi
Matayarisho
Katakata vitunguu na hoho katika vipande vidogo vidogo na kisha kwangua carrot na uweke pembeni.  Chemsha viazi na chumvi kidogo vikiiva viponde na uviweke pembeni, Baada ya hapo tia nyama limao, chumvi, kitunguu swaum na tangawizi ichemshe mpaka iive na uhakikishe maji yote yamekauka. Kisha Tia binzari zote, pilipili, curry powder, giligilani, vitunguu, hoho na carrot. Pika mchanganyiko huo kwa muda wa dakika 3 na kisha ipua. Baada ya hapo changanya na viazi kisha tengeneza maduara ya kiasi na uyaweke pembeni. Chukua unga wa ngano kiasi na uchanganye na maji kupata uji usiokuwa mzito au mwepesi sana. baada ya hapo chovya madonge katika huo uji na uyachome katika mafuta. Hakikisha zinaiva na kuwa rangi ya brown na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.Unaweza ukazisevu na chatney yoyote unayopendelea.

8 comments:

  1. I love kachori, nitajaribu hili pishi, Ahsante kwa kutujuza

    ReplyDelete
  2. hii sio kachori bali ni catles tunavyojua kachori hazina nyama kabiiisa na ikitiwa nyama basi huo ni upishi mwengine nao ni katles

    sio kama najifanya najua ila huo ndio ukweli msipotoshe jina la kachori nasie pia wapishi

    ReplyDelete
  3. Asante sana mdau kwa comment.Ni vizuri ukatambua kwamba kuna aina nyingi za kachori. na hiyo inatokana na filling unayoitumia. Unaweza kutumia nyama na unaweza kutumia vegetable.Na sizani kama nimepotosha jina la kachori.sio hilo tu na wakati mwingine unatakiwa uwe mbunifu ktk kupika.Hiyo ni pure kachori.

    ReplyDelete
  4. aah wapi umechemsha hiyo ni katless bwana.....kachori haina nyama

    ReplyDelete
  5. Waswahili wanakwambia tembea uone, Na kama unabisha kwamba hakuna kachori za nyama Nenda Google kisha andika meat kachori usome.

    ReplyDelete
  6. Yes I agree kuna za nyama na zisizo na nyama. Dunia kitabu usipotembea umesoma just one chapter. Sijui kwanini ana hashed hivyo. Kila mtu ni mpishi lakini ubunifu ndio unatofautisha kati ya mpishi asilia na mpishi wa kukariri.

    Anyway naomba uniambie viazi mbatata ni viazi gani? Ni sweet potatoes au ni vipi hivyo. Nataka nizitengeze over the weekend.

    ReplyDelete
  7. Asante mdau kwa msaada wako wa jibu.
    Viazi mbatata ni hivi viazi vya kawaida ambavyo huwaga tunapikia chips au kwa jina lingine nyumbani tunaviitaga viazi ulaya,na sio sweet potato.
    Plz Utakapozipika tujulishe kama zimetoka vizuri au vip,
    Gudluck.

    ReplyDelete
  8. Nashukuru kwa maelekezo - napenda kuzila ila nilikua sijui jinsi ya kuzipika,

    Shukran.

    ReplyDelete