Monday 9 August 2010

Mapishi ya Viazi utamu na kachumbari




Mahitaji

  • Viazi utamu 3
  • Nyanya 2 kubwa
  • Kitunguu
  • Tango
  • Limao
  • Chumvi
  • Pilipili
  • Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho

Menya viazi na kisha vikate katika vipande. Tia mafuta kwenye chuma cha kukaangia, yakisha pata moto tia viazi nauviache vikaangike mpaka upande mmoja uwe wa brown na kisha geuza upande wa pili na upike mpaka uwe wa brown. Vikisha iva ipua na uweke kwenye kitchen towel ili vikauke mafuta.
Kachumbali: Katakata vitunguu katika bakuli na kisha tia chumvi kwa ajili ya kuondoa ukali wa vitunguu. Baada ya hapo vioshe mpaka chumvi yote iishe. osha nyanya, Pilipili tango na kisha katakata slice nyembamba na uchanganye na vitunguu. Baada ya hapo tia chumvi, kamulia limao na uchanganye zote pamoja   .Baada ya hapo viazi na kachumbali vitakuwa tayari kwa kuliwa.

6 comments:

  1. Nimeipenda sana choice yako ya msosi, keep it up kwani unaongelea vitu ambavyo vinapatikana hata kwenye magenge yetu mtaani.

    ReplyDelete
  2. Mama ntilie tuwekee na mapishi ya futari wenzio

    ReplyDelete
  3. mama ntilie naomba recipe ya pilau mwenzio kila nikipika halinogi

    ReplyDelete
  4. Inapowezekana, naomba majina ya viungo kwa lugha english, kwani wengine majina ya kiswahili ya viungo hatuijui. Shukrani

    ReplyDelete
  5. Asante kwa comment wadau.

    Kwa mdau wa futari,Tafadhari nifutari gani ungependa recipe zake?

    Kwa mdau pilau nitumie email yako ili nikutumie recipe ya pilau. Natarajia kuja kupublish nitakapokuja kupika pilau baadae.

    Mdau wa recipe in english point yako imechukuliwa na katika mapishi yote niliyopublish kama unahitaji naomba nitumie email ili nikutumie kwa kingereza.

    Email yangu ni Asher-86@hotmail.co.uk

    Asante sana wadau wote kwa mchango wenu.

    ReplyDelete
  6. hapa kila kitu kipo sawa...naona kuna mdau anataka majina ya viungo ktk kimombo....kuna kamusi online we tulia kidogo tu online utaipata...au jaribu hii kamusiproject.org/

    ReplyDelete