Tuesday 10 August 2010

Mapishi ya Mandazi



Mahitaji

  • Unga wa ngano (nusu kilo)
  • Sukari (Kikombe 1 cha chai)
  • Chumvi (nusu kijiko cha chai)
  • Hamira (kijiko kimoja cha chai)
  • Yai (1)
  • Maziwa ya unga (vijiko 2 vya chakula)
  • Butter (kijiko 1 cha chakula)
  • Hiliki (kijiko1 cha chai)
  • Maji ya uvuguvugu ya kukandia
  • Mafuta ya kuchomea
Matayarisho

Tia unga kwenye bakuli kisha tia sukari, chumvi, yai, maziwa ya unga, butter na hiliki kisha uchanganye pamoja mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. Baada ya hapo tia maji ya uvuguvugu kiasi na uanze kuukanda. Ni vizuri ukaukanda kwa muda wa dakika 15 ili kuhakikisha donge lote la unga limelainika vizuri.
Baada ya hapo Tawanyishaa unga uliokwandwa katika madonge 4. Tia unga wa ngano kidogo katika kibao cha kusukumia na uanze kusukuma donge moja katika shape ya chapati na hakikisha haiwi nyembamba sana wala nene sana yani inatakiwa iwe ya wastani.Ukishamaliza kusukuma unatakiwa ukate shape uipendayo na uyatandaze katika kitu kilichopo flat na kiwe kimenyunyuziwa unga wa ngano ili kuyazuia yasigandie. Rudia hiyo process kwa madonge yote yaliyobakia. Baada ya hapo yaweke mandazi katika sehemu iliyokuwa na joto ili yaweze kuumuka (inaweza kuchukua masaa 3 kuumuka). Yakisha umuka unatakiwa uweke mafuta katika karai la kuchomea. Yakisha pata joto la kiasi unatakiwa utumbukize mandazi na unaze kuyachoma mpaka yawe ya brown. Yakisha iva yaipue na uyaweke kwenye kitchen towel iliyakauke mafuta. Yakisha poa yatakuwa tayari kwa kuliwa. 

12 comments:

  1. Hongera kwa kuanzisha blog hii kwani tutajifunza mengi kutoka kwako.

    Umeongelea kitchen towel, ni nini naomba unielekeze

    ReplyDelete
  2. Kitchen towel ni tissue inayotumika jikoni. Iko kama toilet paper ila yenyewe ni kubwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa kifupi umenijuza sana mana nimehangaika sana kupika maandazi hadi nilianza kukata tamaa lakini sasa nimeelewa...big up sana mamiii!!!!!!

      Delete
  3. Tumaomba pia maelekezo ya kutayarisha chapati kwa undani. zilizo soft na pia zinazoweza kutumika kwa muda mrefu (zaidi ya siku tano).
    Pia naomba maelezo kidogo kuhusu mafuta ya kupikia, kwani naona kuna ya aina nyingi sana, sunflower, corn, rapeseed oil etc, na ni yapi unapendekeza katika kila menu.

    Naomba tafsiri ya hamira na hiliki pia kwa mahitaji ya hapo juu.

    KK

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  5. Asante mdau KK

    Natumaini kupublish chapiti hapo mbeleni. Ukitaka recipe zake ahead of time, tafadhali naomba unitumie email nitakujibu na maelekezo yote.

    Mafuta ya kupikia ni 'Vegetable oil' au 'sunflower oil' yote ni mazuri tu.

    Hamira kwa kingereza ni 'yeast' na hiliki ni 'cardamon' hii unahitaji iliyosagwa.

    Wako

    Mama Ntilie

    ReplyDelete
  6. Unayo e-mail yangu, subject "tafsiri", naomba chapati recipe, should try it over the weekend...
    Nitaanza accumulate hizi spices sasa, sio tu mixed spice....

    ReplyDelete
  7. Tunaomba maelekezo ya chapati za kusukuma pia.maana wengne tunapika chapati watoto wanachukua wanaendesha kama matairi ya gari zilivo ngumu.unatusaidia sana na hii blog,tunashukuru sana.

    ReplyDelete
  8. Kwa mdau wa chapati za kusukuma. Natarajia kuzipika weekend hii kwahiyo nategemea kupublish on monday. kaa mkao wa kusubiri

    ReplyDelete
  9. NAOMBA UTUFUNDISHE NAMNA YA KUANDAA CHAPATI ZA KUSUKUMA AMBAZO NI LAINI KAMA KEKI paulakwilini@gmail.com

    ReplyDelete
  10. Mama Ntilie hapo juu ... kama hamira yangu ni ya unga nafanyaje? Je nachanganya pamoja na mchanganyiko wa kwanza au?

    ReplyDelete
  11. naomba kutumiwa recipe mpya kila unapotoa.pia sijaona mahali pa ku subscibe ili napata direct.lucy

    ReplyDelete