Friday 6 August 2010

Mapishi ya Mchemsho wa ndizi na nyama



Mahitaji

  • Ndizi mbichi 6
  • Nyama ya ng'ombe (nusu kilo)
  • Viazi mviringo 2
  • Kitunguu swaum
  • Tangawizi
  • Kitunguu maji
  • Nyanya 1 kubwa
  • Mafuta (vegetable oil)
  • Chumvi
  • Limao
  • Pilipili
Matayarisho

Chemsha nyama na limao, kitunguu swaum, tangawizi chumvi na maji kiasi mpaka nyama iive, Hakikisha unaiacha na supu kiasi kwa ajili ya kuwekea kwenye ndizi.Kisha katakata nyanya na vitunguu na uweke pembeni .Menya ndizi na viazi kisha zichemshe pamoja na vitunguu, nyanya, maji kidogo, mafuta  na uhakikishe haziivi kabisa. Baada ya hapo tia nyama na supu yake, pilipili mzima na chumvi na uache uchemke mpaka ndizi na viazi viive.Na baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa

5 comments:

  1. Nimependa sana mcehsho wako jinsi ulivyoupangilia ila kama mimi napenda chakula kama ni mchemsho uwe mchemsho kweli sio tena kuweka mafuta, nadhani mafuta ya nyama yanatosha. Sio nakukosa ila napenda tuwe na ushirikiano katika kuendeleza mapishi ya kitanzania kama nami nimekosea naomba mnikosoe kuhusu kuweka mafuta kwenye mchemsho.

    Nakuaminia Mama Ntilie

    ReplyDelete
  2. Asante sana mdau kwa comment yako, aidia yote ya hii blog ni kubadilishana mawazo ya kiupishi. Nashukuru kwa mchango wako.

    ReplyDelete
  3. Tafadhali waeleze watu aina ya ndizi. Kuna ndizi nyingine haziivi haraka has ndizi zinazoliwa na ndugu zetu wa Rungwe (amatoki in nyakyusa)

    Nadhani ndizi za kagera ni bora kwa upishi wako, nasema hivyo kwa sababu ulishaanza kupika nyuama hivyo ukiitia kwenye ndizi za kinyakyusa zitachukua muda kuiva, nyama inaovercook nadhani na viai pia.

    ReplyDelete
  4. nimefurahiya mchemsho na mimi naenda kujaribu leo

    ReplyDelete
  5. Nimependa maelezo yako kuhusu kutayarisha mchemsho na maoni aliyotoa mdau kuhusu kuweka mafuta zaidi ya yaliyopo kwenye nyama.kuhusu ugumu wa ndizi,nona ni bora usiivishe sana nyama kama unajua ndizi unazotumia ni ngumu.Hii itawezesha nyama kuiva kwa kiasi mara baada ya kuchanganya na ndizi na kufanya mchemsho kuwa na radha nzuri.Mchemsho unakuwa mzuri pale supu inapochanyanyika vizuri na ndizi na kuzipa radhaa(taste)

    ReplyDelete