Sunday 29 August 2010

Jinsi ya kupika Mkate wa sinia



Mahitaji

  • Unga wa mchele (rice flour 2 vikombe vya chai)
  • Sukari (sugar 3/4 ya kikombe cha chai)
  • Hamira (dried yeast 3/4  kijiko cha chakula)
  • Hiliki (cardamon powder 1/2 kijiko cha chai)
  • Ute wa yai 1(egg white)
  • Tui la nazi (coconut milk kikombe 1 na 1/2 cha chai)
  • Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Changanya unga wa mchele, hamira, hiliki na tui la nazi pamoja katika bakuli la plastic kisha koroga vizuri. Ufunike na uwache katika sehemu ya joto mpaka uumuke.(ambayo inaweza kuchukua kama dakika 30-45. Ukisha umuka tia sukari na ute wa yai kisha ukoroge vizuri. Baada ya hapo washa oven katika moto wa 200°C kisha chukua chombo cha kuokea na ukipake mafuta na umimine  mchanganyiko. Kisha utie katika oven na uoke kwa muda wa dakika 40. Hakikisha unaiva na kuwa rangi yabrown juu na chini. Na hapo mkate utakuwa tayari.

4 comments:

  1. aiesee nimejirambaaa,nimepika mkate umetoka bombaaaaaaaa kichizi .Asante kwa Recipe.

    ReplyDelete
  2. Nimefurahi kupata hii habari, lengo letu ni kufundishana namna tofauti za kupika. Karibu sana Mdau.

    ReplyDelete
  3. Hujambo Mama Ntilie,

    mimi pia nimepika mkate ulivyo eleza hapa na umekuwa mzuri sana zaidi. Sija wahi kula mkate tamu kama huu. Mimi ni Mkenya lakini naona sisi wote watoto wa Mungu na nimfurahi sana kupata hii blog yako na recipes timamu. Next on my list: biriani...nitakuambia ilivytokea. Asante tena kwa recipe na Mola akubariki

    ReplyDelete
  4. jamani mimi hapo mgeni, naweza kuweka sufuria kwenye oven maana hivyo vifaa vya oven sina

    ReplyDelete