Saturday, 28 August 2010

Mapishi ya Bagia dengu



Mahitaji

  • Unga wa dengu (gram flour 1/4 kilo)
  • Kitunguu kilichokatwa (onion 2)
  • Hoho (green pepper 1/2)
  • Pilipili iliokatwakatwa (scotch bonnet pepper 1/2)
  • Barking powder (1/4 ya kijiko cha chai)
  • Chumvi (salt)
  • Kitunguu swaum (garlic cloves 2)
  • Mafuta ya kukaangia (vegetable oil)
  • Binzari manjano (turmeric 1/4 ya kijiko cha chai)
Matayarisho
Changanya unga, chumvi, binzari, barking powder kwanza kisha weka maji kiasi na vitu vyote vilivyobakia (isipokuwa mafuta) na ukoroge vizuri kuhakikisha unga hauna madonge.Hakikisha unga hauwi mzito wala mwepesi sana. Kisha uache kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo choma bagia katika mafuta. Ukiwa unachoma hakikisha bagia zinakuja  juu ya mafuta na hazigandi chini. Ikitokea zinaganda chini hapo itakuwa umekosea kitu. Pika mpaka ziwe za light  brown kisha zitowe na uziweke katika kitchen towel ili zikauke mafuta na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

3 comments:

  1. Mama Mtilie, Hii recipe nzuri sana na ningeomba iwe mwanzo wa menu zinazoweza kutumiwa kuwatayarishia watoto wa shuleni day meals ambazo zinaweza kuwa cold. Hii najua ni ishu inawasumbua wazazi wengi kwani ukishatayarisha sandwiches kila siku mtoto ataichoka, na ni vyema uwe na options kadhaa kwa hayo matumizi.
    Nadhani recipe ambazo unaweza kutayarisho once a week na kutumika for that period.
    KK

    ReplyDelete
  2. Kwa mdau mama Jeremiah
    Nitajitahidi kulifanyia kazi ombi lako la mapishi yasiyotumia dairy products na gluten.
    Unga wa dengu unaitwa gram flour.

    ReplyDelete
  3. Asante mama Ntilie, nasubiria kwa hamu..
    Leo ngoja nipike hizi bagia za dengu. Nimepata unga. Asante sana

    ReplyDelete