Mahitaji
- Kunde (Ila mimi nilitumia Nigerian brown beans 1/2 kilo)
- Vitunguu maji (onion 2)
- Pilipili (scotch bonnet pepper 2)
- Vitunguu swaum (garlic 4 cloves)
- Chumvi (salt)
- Barking powder (1/2 kijiko cha chai)
- Machicha ya nazi (grated coconut 1 kikombe cha chai)
- Limao (lemon 1)
- Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Loweka kunde usiku mzima kisha ziondoe maganda na uzitie kwenye blender pamoja na vitunguu maji, vitunguu swaum, pilipili, chumvi,barking powder na maji kiasi. Visage vitu vyote mpaka viwe laini na kisha uutoe na kuweka kwenye chujio ili uchuje maji. baada ya hapo zikaange katika mafuta mpaka ziwe za brown na uzitoe na kuziweka kwenye kitchen towel ili zichuje mafuta.Baada ya hapo saga machicha ya nazi,limao, pilipili chumvi pamoja na maji kidogo na hapo chatney yako itakuwa tayari kwa kuseviwa na bagia.
Habari za leo Mama Ntilie,
ReplyDeleteNi mara ya kwanza kuingia kwenye hii blog yako. NImefurahia mapishi na sasa hivi nipo najaribu kupika mkate wa sinia.
Shida yangu mimi ni kama una recipe za mapishi yasiyo tumia dairy products and are gluten free. Nina mtoto (3yrs) ana allergy ya vitu hivyo. Kama mama, ninahangahika kweli kupata vitu vya kama snacks ili nimpikie.
basi nakutakia siku njema na asante kwa kutuelimisha
Ohh samahani, nimetuma comment kwenye chakula tofauti.. Sikuwa na jinsi ya kukufikishia ujumbe.
ReplyDeleteAsante kwa recipes za bagia.. Nitautafuta unga wa dengu. Je in English is it Chick pea or peas flour?
kazi njema
Ni mimi tena mama Jeremiah
Asante mama ntilie kwa pishi zuri
ReplyDeleteNaulizia jinsi ya kuondoa maganda hizo kunde, je unatumia mikono ama? Shida yangu ni kupata njia itakayo tumia muda mfupi.
Mama Tina.
Asante mama ntilie kwa pishi zuri.
ReplyDeletenaulizia jinsi ya kuondoa maganda hizo kunde, Je unamenya kwa mikono ama?
Shida yangu ni kupata njia itakayo tumia muda mfupi.
Mama Tina
Asante Mama Tina,njia rahisi ya kuondoa maganda Kwa ninayotumia mimi hizi 2.
ReplyDeleteYa kwanza nikisha ziroweka usiku mzima huwa nazitia maji kiasi kisha nazifinyanga na mikono kisha najaza maji utaona maganda yanakuja juu kwa hiyo unamwaga yale maji na maganda Unarudia hilo zoezi mpaka utakaporidhika nazo.
Ya pili ni huwa nazisaga kunde zikiwa kavu katika blenda mpaka zinakuwa machenga kiasi, kisha nazitia kwenye bakuli pana kisha nazifungulia maji bombani yenye pressure kubwa, kama mwanzo kisha utaona maganda yote yankuja juu, unamwaga maji yenye maganda unaendelea kufanya hivyo mpaka maganda yote yatakapoisha.
Jaribu hizo zinaweza ukusaidia.
safi sana nimejaribu kupika ni tamu hizooo
ReplyDeletehabari mama mpishi,naomba unielezee kiungo kinachoitwa thomu ndo kikoje?
ReplyDelete