Mahitaji
- Mchele
- Kisamvu kilichotwangwa
- Samaki
- Mbaazi
- Nyanya chungu
- Vitunguu
- Nyanya ya kopo
- Tangawizi
- Kitunguu swaum
- Vegetable oil
- Curry powder
- Tui la nazi (kopo 2)
- Chumvi
- Pilipili
- Limao
Matayarisho
Safisha samaki kisha wamarineti na kitunguu swaum, tangawizi, pilipili, chumvi na limao kwa muda wa masaa 3.Baada ya hapo wakaange na usiwakaushe sana na uwaweke pembeni kwa ajili ya kuungwa.Katakata vitunguu maji, saga tangawizi na kitunguu swaum. Baada ya hapo injika sufuria ya mchuzi jikoni na mafuta kiasi ya kupikia, mafuta yakisha pata moto, tia vitunguu maji na vikaange mpaka viwe vya rangi ya brown. kisha tia kitunguu swaum na tangawizi.kaanga kidogo kisha tia nyanya ya kopo moja na ufunike. acha mpaka nyanya ziive. Kisha tia chumvi na curry powder na uache ikaangike kwa muda wa dakika 2 kisha tia samaki na nyanya chungu nakisha kamulia nusu ya limao. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia tui la nazi kopo moja na uache ichemke mpaka mchuzi uive.
Baada ya hapo chemsha kisamvu pamoja na mbaazi Kikisha iva, kaanga kitu na nyanya pembeni mpaka ziive kisha tia kisamvu. geuza mchanganyiko mpaka uchanganyike vizuri kisha tia tui la nazi na chumvi na aacha ichemke mpaka tui liive kisha ipua.malizia kwa kupika wali ambapo utachemsha maji kisha tia mafuta,chumvi na mchele na uupike mpaka uive kisha sevu na mboga ulizopika na mlo wako utakuwa tayari kwa kuliwa.
Nashukuru kwa kutuwekea blog ya mapishi, mimi ni mpenzi sana wa kupika.
ReplyDeleteSamahani kwa upande wangu sijapendezewa na mapishi ya wali, samaki na kisamvu, sina maana kuwa haviendani ila kuunga tui la nazi kwenye samaki kisha ukaunga tena kisamvu na tui la nazi naona kama sio vizuri. Nadhani kisamvu kingeungwa na mafuta na samaki ukaunga nazi au kinyume chake samaki akaungwa na mafuta na kisamvu ukaweka tui la nazi.
Ni hayo tu kutoka kwangu, naomba uendelee kutupa aina mbali mbali za madiko diko.
Asante sana mdau kwa mchango wako
ReplyDeleteJamani mafuta na nazi? Chorestrol.
ReplyDeleteNiko pamoja na ma-anoymous hapo juu...Mapishi mazuri lakini mboga mmoja tu ndo iwe na nazi...Au wali wa nazi tu...Asante kwa kutupa maakuli ya kibongo..Hususani sisi mbao tuko mbali na TZ kwa miaka sasa...Kila la kheri mama Nijazie..
ReplyDelete