Monday 2 August 2010

Jinsi ya kupika Eggchop



Mahitaji

  • Mayai yaliochemshwa 4
  • Nyama ya kusaga robo kilo
  • Kitunguu swaum
  • Tangawizi
  • Limao
  • Chumvi
  • Pilipili
  • Breadcrambs
  • Carry powder
  • Binzari nyembamba ya unga
  • Yai moja bichi
  • Mafuta 

Matayarisho

Marinate nyama na pilipili, kitunguu swaum, tangawizi, limao, chumvi, carry powder, binzari nyembamba na breadcrambs pamoja. Kisha vunja yai moja bichi kwenye kibakuli na ulikoroge kisha tia kwenye mchanganyiko wa nyama.Gawanisha matonge manne kwa ajili ya kuzungushia kwenye mayai .Chemsha mayai kwa muda wa dakika 20. Yakisha iva acha yapoe na kisha yamenye maganda na uyaweke pembeni. Baada ya hapo chukua yai moja lililochemshwa na ulizungushie donge moja la mchanganyiko wa nyama. fanya hivyo kwa mayai yote yaliobakia. Baada ya hapo paka mafuta kwa nje ya hizo eggchop na kisha paka mafuta kwenye sinia la kuokea na uziokee kwenye oven kwa moto wa kawaida, kwa muda wa dakika 20.Na eggchop zako zitakuwa tayari kwa kuliwa

13 comments:

  1. hi mama ntilie ningependa kujarib kutengeza egg chop lakin nyama baada ya kutia viungo unaichemsha au itaiva ktk oven?

    ReplyDelete
  2. HONGERA KWA MAPISHI

    ReplyDelete
  3. Nice one, ila tungependa kama ungeweka vipimon ya hivyo viungo,mfano curry kipimo cha curry powder na bizari nyembamba.

    ReplyDelete
  4. Hi, kwanza natanguliza shukrani zangu kwa wote mliotembelea blog yangu na kuweza ku commet pia.

    Majibu nikama ifuatavyo: kwa anonymous no 1
    Nyama baada ya kuitia viungo unaizungungushia tu kwenye yai bila kuchemshwa, na itaivia kwenye oven

    Kwa anonymous no 3
    Asante kwa ushauri wako. Natumai nitaufanyia kazi.

    ReplyDelete
  5. ahsante mimi anonymous no 1 naitwa Hasna napenda sana mapishi ya nyumbani na ni mpishi mzuri sana endelea na libeneke sister.maakuli muhim ktk nyumba kila la kheri

    ReplyDelete
  6. aisee...mpaka nasikia njaa duh!

    ReplyDelete
  7. Mdau Hasna
    ahsante sana kwa comment yako,Ningependa ushirikiano na ingekuwa vizuri kama ungenitumia recipe zako za mapishi ili tu-share na wadau wote.

    ReplyDelete
  8. Hi mama Ntilie,Mzima weye,mimi naitwa Hamisa napenda kupika sana na nakushukuru kwa hii blog yako kwani ninachotaka kupika nakuja hapa kwenye computer naprit paper naenda jikoni,Jana nilipika eggchopndiyo futar yangu kuu before hapo nilikuwa siijui kuipaka ningeweza na mimi kukutumia mapishi ila camera yangu imeharibiki siwezi kukupostia picha.Asante sana

    ReplyDelete
  9. Kwa mdau Hamisa,
    Nimefurahi sana kusikia unafanyia kazi recipe ninazozitoa hapa. Pia nasubiri kwa hamu ukishatengeneza camera yako unitumie recipe ili tuweze ku-share mapishi na wadau wengine pia.
    Ahsante sana

    Wako mama ntilie

    ReplyDelete
  10. Mama ntilie ahsante sana kwa mapishi. Ila nilipojaribu egg chop kutengeneza kama ulivyoelekeza, zangu zilipasuka na kuweka mayai yote nje mara baada ya nyama kuiva toka kwenye oven. Nimekosea wapi?

    ReplyDelete
  11. Kwa mdau wa eggchop
    Inawezekana kipindi unazizungushia nyama hukuweka ya kutosha ndomana zikaweka mayai nje.Ikitokea unajaribu kupika tena, jaribu kuzungushia nyama ya kutosha natumai inaweza kutatua tatizo

    ReplyDelete
  12. Ahsante Mama Ntilie kwa majibu. Ila nafikiri kwa kuweka sawa maelezo yangu ni kwamba nyama niliyoweka ilikuwa ya kutosha. kilichotokea ni kwamba, nyama ilidondokea kwenye tray na mayai yakawa peke yake. Yaani ile nyama haikukamatana sawasawa na mayai. Bila ya shaka sasa utakuwa umeelewa na kunielekeza ipasavyo. Thanks.

    ReplyDelete
  13. Kwa mdau wa eggchop
    Nyama kushika katika mayai inategemeana na uwekaji wa breadcrams na yai(bichi)Ukiwa unapika eggchop unatakiwa uwe unavi adjust mpaka utakapopata matokeo mazuri.Kama nilivyosema ukiwa unakupika unatakiwa ujaribu tena na tena mpaka utakapofanikiwa kwa hiyo usife moyo.

    ReplyDelete