Sunday, 1 August 2010

Mapishi ya Wali, samaki, bilinganya na spinach


Mahitaji

  • Samaki
  • Spinach
  • Bilinganya
  • Nyanya ya kopo (Kopo 1)
  • Vitunguu maji
  • Vitunguu swaumu
  • Tangawizi
  • Pilipli mbuzi
  • Chumvi
  • Limao
  • Carry powder
  • Mchele
  • Mafuta ya kupikia
  • Coriander
  • Hiliki
  • Amdalasini
  • Karafuu

Matayarisho

Osha samaki na kisha wamarinate na vitunguu swaumu, tangawizi, limao, chumvi na pilipili kwa muda wa masaa matatu. Baada ya hapo wakaange samaki na uwaweke pembeni kwa ajili ya mchuzi.
Osha spinach na kisha zikatekate na ziweke pembeni
Osha mchele na kisha uloweke kwenye maji kwa muda wa dakika kumi
Osha bilinganya kisha likatekate vipande vidogo dogo

Jinsi ya kupika

Mchuzi
Saga pamoja vitunguu maji, vitunguu saumu, tangawizi, nyanya.Kisha weka mchanganya katika sufuria na uinjike jikoni kwenye moto wa kawaida. Pika mchanganyiko mpaka ukauke kisha tia mafuta, chumvi na carry powder. pika kwa muda wa dakika kumi kisha tia samaki na tui la nazi. Acha mchuzi uchemke mpaka tui la nazi liive.kishaipua na tia coriander

Spinach
Kaanga vitunguu maji na mafuta, baada ya hapo tia spinach na chumvi acha ziive kidogo kisha ipua tayari kwa kuliwa.

Mabilinganya
Kaanga vitunguu maji na mafuta mpaka viwe vya brown kisha tia nyanya. Acha ziive kisha tiai mabilinganya na chumvi. Yakishaiva ipua weka pembeni tayari kwa kuliwa.

Wali
Chemsha maji ya wali kwenye sufuria, kisha tia hiliki, pilipili mtama mzima, karafuu na amdalasini, chumvi na mafuta. Kisha tia mchele na uufunike na uache uchemke mpaka utakapokauka maji. Geuza na uache mpaka uive. Kisha ipua. Tayari kwa kuliwa

2 comments:

  1. asante kwa kutufundisha mapishi mazuri.

    ReplyDelete
  2. sio watu wote wanakula nyama, je unampango wowote wa kuelekeza jinsi ya kupika vyakula vya wasiokula nyama, samaki, mayai? yaani vegetarian

    ReplyDelete