Monday 16 August 2010

Mapishi ya Chapati za Kusukuma





Mahitaji
  • Unga wa ngano (plain flour 1/2 of kilo)
  • Siagi (butter vijiko 2 vya chakula)
  • Yai (egg 1)
  • Chumvi (1/2 ya kijiko cha chai)
  • Hiliki (ground cardamon 1/4 ya kijiko cha chai)
  • Maji ya uvuguvugu (warm water)
  • Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho
Weka unga wa ngano katika bakuli la kukandia, kisha tia chumvi na  hiliki na uchanganye kwanza, baada ya hapo tia siagi na uichanganye vizuri na unga mpaka ipotee. Baada ya hapo tia tena yai na uchanganye vizuri. Mchanganyiko ukishachanganyika vizuri sasa unaweza kutia maji ya uvuguvugu kidogo, kidogo huku ukiwa unauchanganya ili kupata donge. Baada ya hapo anza kukanda hilo donge mpaka mabuje yote yapotee na unga uwe mlaini, ambapo itakuchukua kama dakika 15. Baada ya hapo tawanyisha unga katika madonge ya wastani (yasiwe makubwa sana au madogo sana) Ukimaliza hapo, andaa kibao cha kusukumia chapati kwa kukitia unga kidogo ili chapati isinatie kwenye kibao. Sukuma donge moja la chapati mpaka liwe flat na kisha weka kijiko kimoja cha mafuta na usambaze. ukisha maliza ikunje (roll). Fanya hivyo kwa madonge yote yaliyobakia.
Baada ya hapo andaa chuma cha kuchomea (fry-pan) katika moto wa wastani. Kisha anza kusukuma chapati (ni vizuri ukaanza na zile ulizozikunja mwanzo ili kuzipa nafasi zile za mwisho ziweze kulainika) ukiwa unasukuma hakikisha zinakuwa flat (na zisiwe nene sana au nyembamba sana) Ukishamaliza hapo tia kwenye chuma cha kuchomea. Acha iive upande mmoja then igeuze upande wa pili. Tia mafuta ama kijiko kimoja kikubwa upande wa chini wa chapati na uanze kuukandamiza kwa juu uku ukiwa unaizungusha. fanya hivyo uku ukiwa unaigeuza kuiangalia kwa chini ili isiungue. ikishakuwa ya brown, geuza upande wa pili na urudie hivyohiyvo mpaka chapati iive. Rudia hii process kwa chapati zote zilizobakia.

Siri ya chapati kuwa laini ni kutia siagi au mafuta ya kutosha kipindi unazikanda na pia kuzikanda mpaka unga uwe laini.

8 comments:

  1. Hi, je naweza kanda unga wa chapati ngumu kwa kutumia bread maker ukiwa tayari nakata madonge na kuendelea na process nyingine

    ReplyDelete
  2. Nakuomba unisaidie recipe ya fried chicken wings

    ReplyDelete
  3. Ndiyo unaweza kukanda unga wa chapati kwakutumia bread maker

    ReplyDelete
  4. Euston we have a major problem.
    Nimejikwaa kujaribu chapati and though edible, still very very hard, Please help this sinking ship.
    Nimejaribu kufuata all directions, lakini sijui kosa liko wapi.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa Euston pole kwa yaliyokukuta. Kuhusu chapati kuwa laini inatokana na ukandaji na pia matumizi ya mafuta/siagi katika ukandaji. Labda jaribu,Na pia ukiwa unakanda unga badala ya kutumia siagi jaribu kukandia mafuta tu (vegetable oil) na ukisha kanda unga wa chapati uweke kwenye bakuli la plastic na uufunike kwa muda wa saa moja kabla yakuanza kuzikunja tena na mafuta. Nakisha kuzisukuma na kuanza kuchoma. Natumai hiyo inaweza kusaidia

    ReplyDelete
  6. Euston, the eagle has landed!
    Mama Ntilie, at long last success on second attempt. Natumai several runs will be an expert. Sikutumia yai na siagi na niliuacha kwa muda mrefu as adviced na sasa inatia moyo for me to attempt the other recipes.

    Thanks again

    ReplyDelete
  7. Kwa mdau Euston,
    Nimefurahi sana kusikia umefanikiwa kuzipika ktk second attempt.Siri ya Mapishi ni kujaribu na sio kufa moyo endapo kitu kinaenda wrong.Kama nilivyosema idea ya blog hii ni kufundishana, so endapo ikitokea unatatizo lolote ktk maswala ya upishi. Feel free kuniuliza swali lolote nami nitakujibu.
    Asante

    ReplyDelete
  8. nimeona njia zote ila mafuta au siagi inakuwa ya moto au baridi?

    ReplyDelete