Tuesday 31 August 2010

Mapishi ya Biriani



Mahitaji

  • Mchele (rice 1/2 kilo)
  • Nyama (beef 1/2 kilo)
  • Vitunguu (onion 2)
  • Kitunguu swaum (garlic 1 kijiko cha chai)
  • Tangawizi (ginger 1 kijiko cha chai)
  • Maziwa mgando (yogurt 1 kikombe cha chai)
  • Hiliki nzima (cardamon 6)
  • Amdalasini nzima (cinamon stick 2)
  • Karafuu nzima (cloves 6)
  • Pilipili mtama nzima (black pepper 8)
  • Curry powder 1/2 kijiko cha chai
  • Binzari manjano (turmaric 1/2 kijiko cha chai)
  • Binzari nyembamba nzima (cumin 1/4 kijiko cha chai)
  • Chumvi (salt)
  • Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia nyama na uikaange kwa muda wa dakika 10. baada ya hapo tia tangawizi, kitunguu swaum, hiliki(4), amdalasini (1), karafuu (4), pilipili mtama (5), Curry powder, binzari manjano, binzari nyembamba na chumvi. Kisha koroga. Baada ya hapo tia yogurt na uipike mpaka ikauke kisha tia maji kidogo, funika na upunguze moto na uache ichemke kwa muda wa nusu saa.Baada ya hapo nyama itakuwa imeiva na mchuzi kubakia kidogo.Kwahiyo itatakiwa kuiipua.
Loweka mchele kwa dakika 10. kisha chemsha maji mengi kidogo katika sufuria kubwa. baada ya hapo tia hiliki (2) amdalamsini (1) karafuu(2) pilipili mtama (3) chumvi na mafuta kiasi. acha ichemke kidogo kisha tia mchele.Hakikisha maji yameufunika mchele kabisa na uuache uchemke kwa muda wa dakika 8 tu (kwani hautakiwi kuiva kabisa) kisha uipue na uchuje maji yote katika chujio. baada ya hapo chukua sufuria ya kuokea (baking pot kama unayoiona kweye picha) Kisha weka wali nusu na uusambaze sawia kisha weka mchuzi nyama na mchuzi wake pia utandaze na umalizie kwa kuweka leya ya wali uliobakia. Baada ya hapo ufunike na uweke kwenye oven kwenye moto wa 200°C kwa muda wa nusu saa.na baada ya hapo biriani litakuwa tayari kwa kuliwa.

Shukrani
Asante sana mdau Sharifa kwa recipe yako. Nimeijaribu na biriani  limetoka bomba. Nikaona ni vizuri  kuipublish recipe hii ili na wadau wengine wafaidike na namna nyingine ya kupika biriani. Na kama kuna wadau wengine wana recipe zao na wangependa kushare nasi, si vibaya kama watanitumia nami nitazipublish kwa moyo mkunjufu.
Asante sana.

7 comments:

  1. Asante kwa mapishi yako mazuri ila kitu kimoja hujatuelimisha sisi tusiokuwa na oven au sufuria ya kuokea tufanyeje ili nasisi walalahoi tuweze kunufaika na mafundisho yako ?

    ReplyDelete
  2. Kwa wale wasiokuwa na oven au sufuria ya kuokea, wanaweza kutumia sufuria ya kawaida yenye mfuniko unaokava vizuri na pia hakikisha inakuwa nzito na pia wanaweza kuokea kwenye jiko la mkaa.(nachomaanisha hapa ni kupalilia moto juu na chini)Natumai hii inaweza kusaidia

    ReplyDelete
    Replies
    1. je nikitaka kuweka rangi nitachanganyaje hapo sijaelewa jamani naomba ushauri ili nami nijaribu kupika. Napenda sana birian

      Delete
  3. Mimi napikaga biriani ya aina hii. Cha nyongeza naweza kuchangia ni, ukishatandaza leya ya kwanza ya wali kwenye 'baking port' nanyungunyizia maji shape ya coil niliyoyaloweka kwenye safron kweka rangi alafu na-sprinkle gilgilani alafu ndio natandaza mchuzi alafu naweka laya ya wali kwa juu na kurida process hle ya kunyungunyiza maji ya safron na gilgilani ndiona bake. Biriani linatoka na wali mwingine wenye colour na gilgilani inaleta ladha na harufu nzuri.

    ReplyDelete
  4. hata nami pia huipika hivi hivi ila mie siweki hizo majani ya giligilani naweka vitunguu nilivyovikaanga kila layer huleta harufu nzuri na ladha pia jaribuni na hio

    ReplyDelete
  5. Asante sana mdau nami nitajaribu hivyo

    ReplyDelete
  6. Asante sana kwa mapishi ya biriani yaani huwa napenda sana kujua jinsi ya kupika biriani lakini nilikuwa sijapata wakunielekeza. Sasa naomba kukuuliza hizo rangi ambazo nazionaga kwenye biriani zinawekwaje wakati wa kupika? na je nikiipika lazima tena iwe na rojo yake ya kuoia au inaliwa hivyohivyo.

    ReplyDelete