Wednesday 1 September 2010

Mapishi ya Pasta za cream na uyoga



Mahitaji

  • Pasta (2 na 1/2 vikombe vya chai)
  • Uyoga (mashroom 2 vikombe vya chai)
  • Cream (1 kikombe cha chai)
  • Mafuta (vegetable oil)
  • Kitunguu (onion 1)
  • Chumvi
  • Majani ya basil (dried basil leaves 1/2 kijiko cha chai)
Matayarisho
Chemsha maji ya kutosha kisha tia chumvi na mafuta kidogo katika hayo maji na baadae tia pasta na uzichemshe mpaka ziive kisha uzichuje maji na uziweka pembeni. Baada ya hapo weka mafuta kidogo katika sufuria kisha tia uyoga uliokatwa na uupike mpaka uive. Baada ya hapo tia majani ya basil, chumvi na cream kisha acha ichemke kisha weka vitunguu na upike kwa muda wa dakika 4 kisha malizia kwa kutia pasta. Zichanganye vizuri na mchanganyiko wote kisha zipike kwa muda wa dakika 5. Na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Unaweza kupika nyama ya kuku (chiken breast) iliyokatwa vipande vidogo vidogo kama saizi na shape ya pasta. Vizuri kuikaanga pembeni mpaka iwe brown na kuiva alafu kuimix kwenye chakula baada ya uyoga na vitunguu kuiva alafu unamix cream kumalizia mapishi.

1 comment:

  1. Hii safi sana, mimi natumia pasta sauce na pia hutumia cheese. This is a good addition to my arsernal of quick meals.

    ReplyDelete