Friday 10 September 2010

Mapishi ya Wali na stuffed pepper



Mahitaji

  • Pilipili hoho (Red pepper 3)
  • Cougette 1
  • Kitunguu  (onion 1)
  • Uyoga (mashroom 1 kikombe cha chai)
  • Carrot 1
  • Nyanya  (fresh tomato 1)
  • Nyanya ya kopo iliyosagwa (tomato paste 3 vijiko vya chai)
  • Giligilani (fresh coriander)
  • Binzari manjano (Turmaric 1/2 ya kijiko cha chai)
  • Curry powder 1/2 ya kijiko cha chai
  • Chumvi (salt)
  • Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Kata hoho kati na utoe moyo wake kisha ziweke pembeni, Kisha katakata cougette, kitunguu, uyoga, carrot, nyanya katika vipande vidogo vidogo, Weka sufuria jikoni na uanze kupika uyoga kwa muda wa dakika 5, kisha weka curry powder, turmaric na chumvi na kaanga kidogo kisha weka vegetable zilizobakia pamoja na nyanya ya kusaga pamoja na giligilani. Zikaange kwa muda wa dakika 5 kisha zitie kwenye hoho na kisha uzibake kwa muda wa dakika 20 na hapo zitakuwa tayari kuseviwa na wali.
Wali: angalia katika recipe zilizopita

2 comments:

  1. Najua safari yangu ndefu kidogo kufikia hapa. Nimejaribu maandazi, looks good lakini vita ilikuwa kwenye high temperature ya mafuta. Nimejaribu smallest hob kwenye cooker on half heat na hapo spidi ya kuepua ikapungua. Earlier ones imebidi nizipitishe kwenye microwave for about a minute kuhakikisha dough imeiva.
    Asante kwa hii shule...

    Mdau wa "euston we have a problem"

    ReplyDelete
  2. Nafurahia sana bidii yako asante. Ila unapochanganya kiingereza na kiswahili inakuwa vigumu kuelewa wakati mwingine, kwa mfano ulipoandika tia vegetables katiika pilipili hoho halafu uzibake mimi ilinichukua sekunde kadhaa kujua kuwa una maana ya kuoka.

    ReplyDelete