Hii pia ni moja ya favorite takeaway yangu. Mara nyingi huwaga nikichoka kula vyakula vya kichinese na vya kihindi au nandos huwa napenda kula samaki wa kuokwa katika mgahawa wa kilebanese ninaoupenda. Hapa nili-order samaki wa kuokwa na chips na salad. Huu ni mlo mzuri wa afya isipokuwa chips tu. Kama ukitaka kuoka samaki mzima kama huyu, muhimu tu kumkata miraba kila upande na kum-marinate masaa matatu hadi sita ili aingie viuungo vizuri na kumuoka kila upande dakika kumi katika moto usiokuwa mkali sana.
Mapishi Matamu
Mapishi Matamu ni blog ya kujifunza jinsi ya kupika mapishi mbalimbali ya kitanzania, mapishi ya kiswahili kama mapishi ya wali, Pilau, Biriani. Jinsi ya kupika mboga mbalimbali kama, mapishi ya kuku, samaki, maharage nakadhalika. Pia Mapishi matamu blog ina mapishi ya vitafunio mbalimbali kama, mapishi ya keki, maandazi, vitumbua, kachori nakadhalika.
Wednesday, 5 October 2011
Seabass wa kuokwa na chips (takeaway)
Hii pia ni moja ya favorite takeaway yangu. Mara nyingi huwaga nikichoka kula vyakula vya kichinese na vya kihindi au nandos huwa napenda kula samaki wa kuokwa katika mgahawa wa kilebanese ninaoupenda. Hapa nili-order samaki wa kuokwa na chips na salad. Huu ni mlo mzuri wa afya isipokuwa chips tu. Kama ukitaka kuoka samaki mzima kama huyu, muhimu tu kumkata miraba kila upande na kum-marinate masaa matatu hadi sita ili aingie viuungo vizuri na kumuoka kila upande dakika kumi katika moto usiokuwa mkali sana.
Labels:
Takeaway
Wednesday, 28 September 2011
Mapishi ya samaki aina ya salmon
Wakati mwingine mtu unakuwa umechoka na usingependa kupoteza muda jikoni, so mlo wa chapchap unakuwa ni wazo zuri, Mlo huu ni rahisi kuuanda na hata haikuchukui zaidi ya dakika ishirini chakula kinakuwa tayari mezani.
Mahitaji
Salmon fillet 2Potatao wedge kiasi
Lettice kiasi
Cherry tomato
Limao 1
SwaumChumvi
Olive oil
Matayarisho
Mmarinate samaki na chumvi, swaum na nusu ya limao kisha muweke pembeni, baada ya hapo washa oven kisha tia potato wedge zikisha karibia kuiva anza kumpika samaki, tia mafuta kidogo sana kama kijiko kimoja cha chai hivi katika frypan isiyoshika chini yakisha pata moto kiasi muweke samaki wako (upande wenye ngozi chini kwanza) Mpike mpaka uone rangi ya kahawia kwa chini kisha mgeuze upande wa pili, uku samaki wako akiwa anaendelea kuiva, tayarisha salad yako kwa kusafisha lettice na nyanya kisha zichanganye pamoja kisha tengeneza salad dressing pembeni , kamua limao kisha tia olive oil na chumvi kidogo, Baada ya hapo samaki na potato wedge vitakuwa vimeiva, andaa mlo wako na utakuwa tayari kwa kuliwa.
Labels:
Mlo Mkuu
Thursday, 22 September 2011
Mapishi ya mboga mchanganyiko
Mahitaji
Viazi ulaya 4 vya wastani
Hoho jekundu 1/2
Hoho la njano 1/2
Hoho la kiajani 1/2
Njegere 1 kikombe cha chai
Carrot 1 kubwa
Broccoli kidogo
Cauliflower kidogo
Kitunguu 1
Nyanya 1/2 kopo
Swaum/tangawizi 1 kijiko cha chakula
Curry power 1 kijiko cha chakula
Coriander powder 1 kijiko cha chai
Tarmaric 1/2 kijiko cha chai
Olive oil
Chumvi
1/4 ya limao
Matayarisho
Katika sufuria isiyoshika chini kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia swaum/tangawizi na spice zote kaanga kwa muda mfupi kisha tia nyanya na chumvi. pika mpaka nyanya ziive kisha tia vegetable zote na vimaji kidogo sana na kisha kamulia limao, baada ya hapo punguza moto na kisha funika na zipike mpaka vegetable zote ziive na rojo ibakie kidogo. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa.
Labels:
Mboga
Friday, 16 September 2011
Mapishi ya choroko
Mahitaji
Choroko kikombe 1 na nusu
Nazi kopo 1
Kitunguu kikubwa 1
Nyanya 1/2 kopo
Swaum 1 kijiko cha chai
Curry powder 1 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Olive oil
Pilipili nzima
Matayarisho
Loweka choroko usiku mzima kisha zichemshe mpaka ziive na ziweke pembeni. Baada ya hapo saga pamoja nyanya, kitunguu, na swaum kisha vipike mpaka maji yote, baada ya hapo tia mafuta na curry powder, pika mpaka nyanya zitoe mafuta kisha tia choroko,tui la nazi, maji nusu kikombe,pilipili na chumvi, kisha koroga vizuri na uache ichemke. Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na rojo ibakie kidogo sana, kisha ipua na mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Mi huwa napenda kuila na wali ila hata na ugali au chapati inaenda pia.
Labels:
Mboga
Monday, 12 September 2011
Jinsi ya kutengeneza coleslaw
Mahitaji
Kabichi iliyokatwa nyembamba 2 vikombe
Carrot iliyokwaguliwa 1
Kitunguu 1/4 kilichokatwa vyembamba
Yogurt au mayonnise 1/2 kikombe
Limao 1/4
Chumvi kiasi
Matayarisho
Katika bakuli safi changanya vitu vyote mpaka mchanganyiko wako uchanganyike vizuri, kisha iweke frijini kwa muda mchache ili chumvi na limao viingie katika kabichi na carrot. Baada ya hapo caleslaw yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Hii ni moja wapo aina ya salad na mara nyingi pindi watengenezapo hupenda kutumia mayonnise, Ila kwa mimi hupenda kutumia yogurt badala ya mayonnise.kwa maana mayonnise ina mafuta sana. Kwa hiyo hapo chaguo ni lako unaweza tumia mayonnise au yogurt.Unaweza kulia na chips,nyama au chochote upendacho.
Labels:
Salad
Wednesday, 7 September 2011
My favorite takeaway
Lebanese
Kikawaida mimi nikiamuaga kula vyakula vya nje, huwaga napenda kujaribu vyakula kutoka nchi mbalimbali ili kuona ni jinsi gani mapishi yao yako tofauti na yakwetu, na ikitokea nimekipenda chakula chao huwaga natafuta recipe zake na kujaribu kupika mwenyewe nyumbani.
Basi kama uonavyo kwenye picha, kuna wings, ambazo zimemarinatiwa vizuri kisha zikachomwa (grill wings, chips na salad. Hizo wings zao ni tamu kwelikweli.
Labels:
Takeaway
Saturday, 3 September 2011
Mapishi ya Kabichi
Mahitaji
Kabichi 1/2 kilo
Nyanya ya kopo 1/2
Kitunguu 1
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Chumvi
Olive oil
Matayarisho
Kwanza kabisa bandua magada ya juu ya kabichi, kisha ioshe na uikaushe maji baaba ya hapo katakata kabichi (inapendeza zaidi kama ikikatwa nyembamba) kisha saga pamoja nyanya na kitunguu. Baada yahapo tia katika sufuria ya kupikia, ipike mpaka maji yote yatakapokauka kisha tia chumvi, curry powder na mafuta pika kwa muda kiasi kisha tia kabichi na upunguze moto. Pika mpaka kabishi itakapoiva kisha ipua na itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila kwa wali au ugali.
Labels:
Mboga
Subscribe to:
Posts (Atom)