Monday, 23 August 2010

Mapishi ya Viazi, samaki na asparagus



Mahitaji

  • Viazi (potato 1/2 kilo)
  • Samaki (fish 2)
  • Asparagus 8
  • Kitunguu kilichokatwa (chopped onion 1)
  • Kitunguu swaum kilichosagwa (garlic 4 cloves)
  • Tangawizi iliyosagwa kiasi (ginger paste)
  • Limao (lemon 1)
  • Giligilani iliyokatwakatwa (chopped coriander)
  • Curry powder (kijiko 1 cha chai)
  • Chumvi (salt)
  • Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Safisha samaki na kisha uwamarinate na kitunguu swaum, tangawizi, limao na chumvi kwa muda wa nusu saa. Baada ya hapo wakaange na usiwakaushe sana kisha waweke pembeni. Chukua fry-pan kisha tia mafuta kidogo sana (kama 1/2 kijiko cha chai) kisha tia vitunguu maji na uvikaange kwa muda wa dakika 2 (kwani havitakiwi kuiva kabisa) kisha waweke samaki na uwachanganye na hivyo vitunguu. Kisha baada ya hapo tia giligilani iliyokatwa, kamulia limao na tia chumvi kidogo kisha geuzageuza ili kuchanganya vitu vyote na kisha ipua. Baada ya hapo menya na ukate viazi katika  vipande vya wastani, na kisha uvichemshe kidogo na visiive kabisa. Baada ya hapo weka sufuria jikoni kwenye moto wa wastani na utie mafuta kidogo (kama vijiko 2 vya chakula) na kisha tia viazi na uanze kuvipika kwa kuvigeuzageuza mpaka viive na kuwa rangi ya brown kisha tia chumvi kidogo, curry powder na giligilani iliyokatwa.Vipike kwa muda wa dakika mbili kisha viipue. Na baada ya hapo malizia kwa kupika asparagus. Kwanza zioshe kisha zikate kati. Baada ya hapo weka mafuta kidogo kama 1/2 kijiko katika fry-pan yakisha pata moto tia kitunguu swaum, asparagus na chumvi.Zipike kwa kuzigeuzageuza kwa muda wa dakika 5 na hapo zitakuwa zimeshaiva na tayari kwa kuliwa pamoja na samaki na viazi. Unaweza kuvisevu kwa ketchup.

4 comments:

  1. Asante dada kwa kutuelimisha, mimi napenda sana kupika nikisoma mapishi hapa jioni naenda kujaribu ila leo nitakwama maana sijui hiyo asparagus nitaipata wapi, naomba msaada, nipo hapa Tz Dsm niende soko gani kariakoo au kisutu ?

    ReplyDelete
  2. Asante sana mdau, nimefurahi sana kusikia unafanyia kazi recipe zangu.Kuhusu asparagus kwa kweli mimi sijui kwa uko Tz zinapatikana maeneo gani maana tangu niishi uko sijawahi kuziona au kuzisikia ila nimekuja kuzijulia uku Uingereza. Jamani kama kuna mdau yeyote anayeishi Tz na anajua ni wapi asparagus zinapopatikana naomba tusaidiane

    ReplyDelete
  3. Nadhani nimeshaziona Shoprite kama sijakosea. Sijawahi kuziona sokoni.
    Asante sana dada kwa hii blog hata mimi inanisaidia sana. Mimi nilikulia nje ya nchi ni nikarudi ukubwani kwahiyo mapishi yakiTanzania huwa nayaogapa maani sina uzoefu nao sana. Lakini hii blog inanisaidia sana. Naomba email yako ili sometimes niweze kukuuliza maswali.

    Thanks

    ReplyDelete
  4. asante sana mdau,nimefurahi sana kusikia hii blog inawasidia wengi. Nazani mdau aliyeuliza asparagus zinapatika wapi kwa uko Tz anaweza kwenda kuziangalia SHOPRITE.Kwa mdau wa pili hii ni email yangu: Asher-86@hotmail.co.uk. Unaweza kuniuliza maswali yote yanayohusiana na upishi.
    Asante

    ReplyDelete