Friday 5 August 2011

Caramel Custard


Mahitaji
Mayai 4
Maziwa kikombe 1
Vanilla 1/2 kijiko cha chai
Sukari 1/2 kikombe cha chai

Matayarisho
Changanya pamoja mayai, maziwa, vanilla na robo ya sukari kisha visage katika blender (kama huna blender unaweza kutumia egg whisk) mpaka vichanganyike vizuri kisha chuja mchanganyiko wako na uweke pembeni. Baada ya hapo chukua sukari iliyobaki na utie vimaji kidogo kisha uipike mpaka ibadilike rangi na kuwa light brown kiasi kisha isambaze vizuri katika hiyo sufuria. Baada ya hapo tia mchanganyiko wako katika hiyo sufuria yenye sukari iliyoyeyushwa, kisha chukua tray ya kubake tia maji kiasi na uiweke sufuria iliyokuwa na mchanganyiko wako juu yake, Ibake kwa moto wa chini mpaka itakapokuwa ngumu inaweza kuchua kama dakika 45 au saa 1. Baada ya hapo chukua sahani pana funika juu yake kisha ipindue sufuria ili kuitoa katika sufuria. Baada ya hapo iache ipoe na hapo itakuwa tayari kwa kuliwa

2 comments:

  1. Kuchuja kivipi? Fafanua.Kuchuja kivipi? Fafanua.

    ReplyDelete
  2. Unachuja mchanganyiko wako na chujio la chai ili kuondoa small pieces of egg shell KAMA ziliingia kipindi unavunja mayai.

    ReplyDelete