Wednesday, 31 August 2011

Bread and Butter pudding
                             

Mahitaji
Slice za mkate  6
Sukari 1/4 kikombe
Mayai 2
Maziwa 2 vikombe vya chai
Zabibu kavu  kidogo
Vanilla 1 kijiko cha chai
Cinnamon power 1/4 kijiko cha chai
Double cream 1/2 kikombe cha chai
Siagi kiasi

Matayarisho
Paka Siagi(butter) slice zote za mkate(upande mmoja tu) kisha ziweke pembeni. Baada ya hapo katika bakuli kubwa changanya pamoja sukari, mayai, maziwa, cream, cinnamon powder na vanilla kisha koroga mpaka mchanganyiko wako uchanganyike vizuri, kisha chukua sufuria ya kubakia ipakaze butter kidogo kisha panga slice zote za mkate, tia zabibu na kisha umwagie mchanganyiko wako wote katika hiyo mikate. Baada ya hapo iache kwa muda wa dakika 20 ili mkate upate kujiloweka katika huo mchanganyiko. Baada ya hapo Ubake kwa moto wa chini kwa dakika 20 uku ukiwa umeifunika, kisha toa mfuniko na zima moto wa chini na uwashe moto wa juu na uibake kwa dakika 20 zingine na pia hakikisha juu unapata rangi ya kahawia. Iache ipowe kidogo Na baada ya hapo pudding yako itakuwa tayari kwa kuliwa.

2 comments:

  1. Habari za siku Mama Ntilie, tupo pamoja ila busy kidogo. Mapishi yako are something else!

    ReplyDelete
  2. Nzuri tu Nancy,
    Kuhusu kuwa bize usijali sana dadaangu kwani naelewa ndo maisha ya siku hizi.
    Anyway,Asante kwa kunijulia hali na nakutakia siku njema

    ReplyDelete