Friday 6 May 2011

Potato and fish casserole





Mahitaji
Viazi (potato) 1/2 kilo
Fillet ya samaki isiyokuwa na mifupa 1 kubwa kiasi
Carrot 1
Maziwa kikombe 1 na 1/2
Unga wa ngano 2 vijiko vya chakula
Kitunguu maji 1 kikubwa
Cheese iliyokwanguliwa 1/4 kikombe
Butter 1 kijiko cha chakula
Curry powder 1/2 kijiko chai
Turmaric 1/4 kijiko cha chai
Tangawizi/ swaum 1/2 kijiko cha chai
Chumvi

Matayarisho
Katakata viazi na carrot katika cubes ndogondgo kisha tia chumvi kidogo sana na uvichemshe kidogo vikikaribia kuiva viipue na uviweke pembeni. Katika sufuria nyingine tia butter ikisha pata moto kaanga vitunguu (visiwe vya brown) kisha tia tangawizi, swaum, chumvi na spice zote. Kaanga kidogo kisha tia unga wa ngano uchanganye vizuri kisha tia maziwa na uache uchemke kidogo uku ukiwa unakoroga(hakikisha unapata uji mzito kiasi kisha ipua na uwadumbukize samaki humo. Baada ya hapo chukua sufuria ya kuokea na utie viazi na hiyo rojo ya samaki, changanya vizuri kisha mwagia cheese kwa juu na ubake kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo chakula chako kitakuwa tayari kwa kuliwa.

2 comments:

  1. looks tamu...! nna swali tutumie cheese aina gani?

    ReplyDelete
  2. Thanks Nancy Ni kweli tamu kwa maana mume wangu huwa anapenda niipike mara kwa mara na pia haichukui muda mrefu jikoni.Kuhusu cheese unaweza kutumia yeyote uipendayo, na kama sio mtumiaji wa cheese haitozuru usipoweka kwani still ita taste tamu vilevile. Pia unaweza kutumia chicken breast badala ya samaki.

    ReplyDelete