Wednesday 11 August 2010

Mapishi ya Ndizi mzuzu



Mahitaji

  • Ndizi tamu (plantain) 3-4
  • Tui la nazi (coconut milk) kikombe 1 cha chai
  • Sukari (sugar) 1/4 ya kikombe cha chai
  • Hiliki (Ground cardamon) 1/4 ya kijiko cha chai
  • Chumvi (salt) 1/4 ya kijiko cha chai
Matayarisho

Menya ndizi kisha zikwangue utomvu wote. Baada ya hapo zikate kati (kiurefu) na kisha kata tena kati katika kila ndizi vitoke vipande 4. baada ya hapo toa moyo wa katikai wa ndizi. Zioshe na kisha zikaushe maji na uziweke kwenye sufuria ya kupikia. Baada ya hapo tia tui la nazi, sukari, chumvi na hiliki. Ziinjike jikono na uziache zichemke uku ukiwa unalikoroga tui ili lisikatike. Baada ya dakika 10 tui la nazi litakuwa limepungua na kubaki kidogo na hapo ndizi zitakuwa zimeshaiva. Ziache zipoe na zitakuwa tayari kwa kuliwa. Zinaweza kuliwa kama mlo (main meal) au kitinda mlo (dissert) au mlo wa pembeni (side dish) haswa kwa futari.

2 comments:

  1. Ni mimi ndio niliyeomba utuwekee mapishi ya futari, napenda ideas zako so far una choice nzuri na chochote utakachoweka ahsante nitakifanyia kazi kwani unaweka vitu ambavyo vinapatikana kwa urahisi.

    ReplyDelete
  2. Nimependa sana mapishi ya ndizi mzuzu.Je,ni zile mbichi au zilizoanza kuiva?

    ReplyDelete