Friday, 16 September 2011

Mapishi ya choroko


Mahitaji
Choroko kikombe 1 na nusu
Nazi kopo 1
Kitunguu kikubwa 1
Nyanya 1/2 kopo
Swaum 1 kijiko cha chai
Curry powder 1 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Olive oil
Pilipili nzima

Matayarisho
Loweka choroko usiku mzima kisha zichemshe mpaka ziive na ziweke pembeni. Baada ya hapo saga pamoja nyanya, kitunguu, na swaum kisha vipike mpaka maji yote, baada ya hapo tia mafuta na curry powder, pika mpaka nyanya zitoe mafuta kisha tia choroko,tui la nazi, maji nusu kikombe,pilipili na chumvi, kisha koroga vizuri na uache ichemke. Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na rojo ibakie kidogo sana, kisha ipua na mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Mi huwa napenda kuila na wali ila hata na ugali au chapati inaenda pia.

2 comments:

  1. Safi sana!!
    Choroko ni tamu sana!!!

    Mapishi safi na umeyaelezea vizuri

    ReplyDelete
  2. yani leo ndo naiona hii blog yako,uwiiii nimeipendaje sasa na nnavopenda pika acha,kesho naenda tafuta choroko mana sijaipika kwa miaka mingi aseee

    asante kwa mapishi haya najifunza pika choroko

    ReplyDelete