Mahitaji
Olives za kijani kiasi
Olives nyeusi kidogo
Limao 1
Swaum punje 3
Uyoga (ambao ni safe kuliwa mbichi)
Olive oil
Chumvi
Hoho jekundu 1/2
Pilipili ya unga 1/4 kijiko cha chai
Dried palsely 1/4 kijiko cha chai
Matayarisho
Katika bakuli safi, safisha uyoga kisha katakata slice nyembamba,pia katakata swam na hoho vipande vidogovidogo. Baada ya hapo tia vitu vyote vilivyobakia na uchanganye vizuri kisha iache kwa muda wa nusu saa ili spice zichanganyike vizuri.Na baada ya hapo olive zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.Hiki ni kitafunwa kizuri ambacho unaweza kula kabla ya mlo mkuu, au unaweza kulia na nyama choma na pia unaweza kukila chenyewe kama kilivyo.
No comments:
Post a Comment