Friday 1 July 2011

Tzatziki


Mahitaji
Tango 1 lilomenywa
Limao 1/4 kipande
Kitunguu swaum 1 punje
Olive oil 1 kijiko cha chai
Chumvi kidogo
Yogurt kiasi

Matayarisho
Kwangua tango katika grater kisha kamua maji yote. Baada ya hapo weka ktk kibao cha kukatia na uchop chop mpaka vitoke vipande vidogovidogo kisha tena kamua maji yote na utie ktk bakuli lilokuwa kavu. Baada ya hapo tia yogurt kiasi, chumvi kidogo,kitunguu swaum (hakikisha umekisaga) olive oil na kisha kamulia limao. koroga kupata paste nzito na hapo tzatzki yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Hii ni dipping source unaweza kuitumia kama kachumbari. Inapendeza zaidi kama ukiilia na pita bread.Sio hivyo tu pia huwa inatumika kama cooler ikiwa umekula vyakula vya pilipili sana kama nyama choma na vinginevyo

5 comments:

  1. Sasa pishi hili tunaliweka kundi (category) gani?

    ReplyDelete
  2. Hii ni dipping source unaweza kuitumia kama kachumbari. Inapendeza zaidi kama ukiilia na pita bread.Sio hivyo tu pia huwa inatumika kama cooler ikiwa umekula vyakula vya pilipili sana kama nyama choma na vinginevyo

    ReplyDelete
  3. Mama Ntilie mie pia ni mpenzi sana wa blog yako. Napenda sana kupika. Mi nilikuwa naomba tu unisaidie kuweka recipe ya chapati. Yaani mi nikipika chapati hazichambuki na zinakuwa ngumu. Nimeshajaribu mbinu zote mpaka ya kukandia na maji ya kwenye freezer nikidhani labda zitakuwa laini ila wapi. Tafadhali nisaidie.

    Shukran.

    Mariam

    ReplyDelete
  4. Asante sana Mariam. Kuhusu recipe ya chapati nilishaweka kipindi cha nyuma cha kufanya ni kwenda kwenye old post utakuta recipe ya chapati.Jaribu mbinu hizo natumai zitakusaidia

    Mama Ntilie

    ReplyDelete
  5. Thnx! Lazima nijaribu hii

    ReplyDelete