Mahitaji
Spinach 1/2 packet au Mafungu 2
Egusi (ground pumpkin seeds) 4 vijiko vya chakula
Dagaa 1/2 kikombe
Nyanya ya kopo (tin tomato) 1/2
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Curry powder 1/4 kijiko cha chai
Kitunguu (onion) 1
Pilipili (scotch bonnet chilli) 1/2
Kitunguu swaum na tangawizi (garlic and ginger paste) 1 kijiko cha chai
Maggi cubes 1
Lemon 1/4
Chumvi (salt)
Mafuta ya kupikia
Matayarisho
Osha,katakata spinach na zikaushe maji kisha ziweke pembeni. Saga pamoja nyanya, kitunguu, pilipili, garlic na ginger kisha tia kwenye sufuria na uvipike mpaka maji yote yakauke.Baada ya hapo tia dagaa,curry powder na mafuta kiasi, Zikaange pamoja kwa muda wa dakika tano na ukamulie limao. Baada ya hapo katika bakuli tia egusi na maji kiasi kisha ikoroge mpaka madonge yote yatoke na uitie kwenye mchanganyiko wako kisha tia maggi cube na maji kidogo na upike kwa muda wa dakika 30 pia mpaka maji yakauke na upate paste nzito.Baada ya hapo Tia spinach na uzipike mpaka ziive, kisha ipua na mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Inapendeza zaidi ukilia na ugali malaiiiini.
Note:
Ukisha tia egusi unatakiwa upunguze moto kwa maana moto ukiwa mkubwa haikawii kushika na kuungua chini. Pia usitie chumvi baada ya kuweka maggi cube kwa maana zina chumvi.kwa hiyo unatakiwa kuonja kwanza kabla ya kuongeza chumvi.
No comments:
Post a Comment