Tuesday, 29 March 2011

Mapishi ya Viazi Ulaya


Mahitaji
Viazi mbatata (potato) 1 kilo
Vitunguu (onion) 2
Kitunguu swaum (garlic paste) 1 kijiko cha chai
Carrot zilizokwanguliwa (grated carrots) 2
Hoho jekundu lilokatwakatwa (chopped red pepper) 1
Hoho la kijani lilokatwakatwa (chopped green pepper) 1
Curry powder 1 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia kiasi
Chumvi (salt)
Fresh coriander kiasi

Matayarisho
Katakata viazi katika vipande vya wastani kisha vichemshe na chumvi mpaka viive kisha viweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu kidogo (visiwe vya brown) kisha tia kitunguu swaum, hoho zote na curry powder. Changanya vizuri na uzipike kwa dakika 2 kisha tia viazi,carrot na chumvi kidogo na vimaji kidogo  uchanganye vizuri na upunguze moto  na kisha vipike kwa muda wa dakika kumi. Baada ya hapo malizia kwa kutia coriander na uipue. Na hapo viazi vyako vitakuwa tayari kwa kuliwa.

Thursday, 24 March 2011

Mapishi ya Kababu (Meatballs)


Mahitaji
Nyama ya kusaga (minced beef) 1/2 kilo
Kitunguu kikubwa (large onion) 1
Kitunguu swaum/ tangawizi (ginger/garlic paste) 1 kijiko cha chakula
Chenga za mkate (Breadcrambs) 3 vijiko vya chakula
Yai (egg) 1
Curry powder 1 kijiko cha chai
Turmaric 1/2 kijiko cha chai
Pilipili ya unga (chilli powder 1/2 kijiko cha chai
Coriander powder 1/2 kijiko cha chai
Giligilani (fresh chopped coriander)
Limao (lemon) 1/2
Chumvi
Mafuta ya kukaangia

Matayarisho
Changanya vitu vyote (kasoro mafuta ) katika bakuli hakikisha mchanganyiko wako umechanganyika vizuri, kisha tengeneza maduara ya wastani na uyahifadhi frijini kwa muda wa masaa 4 (au unaweza kuziacha zimarinate kwa usiku mzima) Baada ya hapo zikaange kwenye mafuta mpakaziive naziwe rangi ya brown. Kisha ziipue na uziweke kwenye kitchen towel ili zichuje mafuta na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
 Pia unaweza kuzibake katika oven kama hutaki kuzikaanga.

Sunday, 20 March 2011

Mapishi ya Samaki wa kuokwa


Mahitaji
Mackerel 2
Kitunguu swaum na tangawizi (ginger and garlic paste) 1 kijiko cha cha kula
Pilipili iliyo katwakatwa (chopped scotch bonnet ) 1/2
Limao (lemon) 1/2
Chumvi (salt) kiasi
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Coriander powder 1/2 kijiko cha chai
Mafuta 1 kijiko cha chai

Matayarisho
Safisha samaki kisha wakaushe maji ( ukipenda unaweza kuwakata kati au ukawapika wazima) Baada ya hapo wakate mistari kila upande ( ili spaces ziweze kuingia ndani) kisha waweke kwenye bakuli na utie spice zote. Wachanganye vizuri kisha waweke frijini na uwaache wamarinate kwa muda wa masaa 3. Baada ya hapo washa oven kisha wapakaze mafuta na uwafunge kwenye foil na uwatie kwenye oven kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo fungua foil na uwaache kwenye oven kwa muda wa dakika 10 ili wapate kukauka kidogo. Na hapo watakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuwala kwa kitu chochote upendacho.

Thursday, 17 March 2011

Jinsi ya kupika Mkate


Mahitaji
Unga wa ngano ( self risen flour) kikombe 1 na 1/2
Hamira (yeast) 1 kijiko cha chai
Sukari (sugar) 1 kijiko cha chakula
Chumvi (salt) 1/2 kijiko cha chai
Siagi iliyoyeyushwa (melted butter) 1 kijiko cha chakula
Maji ya uvuguvugu ( warm water) kiasi

Matayarisho
Changanya vitu vyote katika bakuli kubwa kisha aanza kukanda mpaka upate donge laini.Baada ya hapo liweke hilo donge kwenye bakuli la plastic na weke katika sehemu yenye joto ili unga uumuke. Hakikisha unga unaumuka zaidi (yani unaji double size) unaweza kuchukua kama saa 1 na nusu hivi. Baada  ya hapo ukande tena na uache uumuke tena  kwa mara ya pili, Ukisha umuka pakaza butter katika baking tin (chombo cha kuokea) na upakaze mkate butter kwa juu,kisha uoke katika oven kwa muda wa dakika 30 (katika moto wa 200C) (hakikisha juu na chini unakuwa wa brown  Na hapo mkate wako utakuwa tayari 

Monday, 14 March 2011

Mapishi ya Kofta curry


Mahitaji
Vitu vya kofta
Nyama ya kusaga (minced beef) 1/4 kilo
Yai (egg) 1
Kitunguu maji (chopped onion) 1
Kitunguu swaum/ tangawizi (ginger and garlic paste) 1 kijiko cha chakula
Garam masala powder 1 kijiko cha chai
Pilipili ya unga (chilli powder) 1/2 ya kijiko cha chai
Limao (lemon) 1/2
Breadcrumbs 3 vijiko vya chakula
Chumvi (salt)

Vitu vya curry
Tui la nazi (coconut milk) kopo 1
Nyanya (fresh tomato) 2
Kitunguu (onion) 1
Kitunguu swaum/tangawizi (ginger and garlic paste) 1 kijiko cha chai
Curry powder 1 kijiko cha chai
Coriander powder 1/2 kijiko cha chai
Turmaric 1/2 ya kijiko cha chai
Chumvi (salt)
Mafuta (veg oil) kiasi
Giligilani (coriander)

Matayarisho
Changanya nyama na vitu vyake vyote kisha iache kwa muda wa 1/2 saa ili iingie viungo. Baada ya hapo tengeneza maduara na uyapange kwenye baking tray kisha zichome kwenye oven mpaka ziive. Baada ya hapo saga pamoja nyanya, kitunguu, swaum na tangawizi. kisha vitie kwenye sufuria na upike mpaka maji yote yakauke, kisha weka mafuta kidogo, chumvi na spices zote koroga mpaka vichanganyike vizuri kisha tia tui la nazi. Liache lichemke mpaka libakie kidogo na umalizie kwa kutia kofta. Zichanganye vizuri na huo mchuzi kisha ziache zichemke kidogo na uipue. Malizia kwa ku garnish na coriander na hapo kofta curry yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kula kwa wali, ugali, viazi au chapati.




Friday, 11 March 2011

Mapishi ya Mixed vegetable fried rice (chinese)


Mahitaji
Wali uliopikwa (cooked rice) kiasi
Hoho la kijani (green pepper) 1/2
Hoho jekundu (red pepper) 1/2
Carrot 1
Kitunguu kikubwa (onion) 1
Njegere (pears) 1/2 kikombe cha chai
Mayai (eggs) 2
Uyoga (mushroom) 2 vikombe vya chai
Soy source 2 vijiko vya chakula
Chumvi (salt) kiasi
Mafuta (veg oil) 3 vijiko vya chakula

Matayarisho
Katakata hoho, kitunguu,na uyoga vipande vikubwa kiasi(chunks) kisha katakata carrot zisiwe nene au nyembamba sana. Baada ya hapo weka mafuta katika katika frying pan yako isiyoshika chini acha yapate moto kisha tia uyoga na ukaange mpaka uive.Baada ya hapo tia vegetable zote na uzikaange pamoja na uyoga kwa muda wa dakika 2, kisha katika hiyohiyo frying pan zisogeze vegetable zako pembeni (ili kupata nafasi ya kukaangia mayai).Yakaange mayai katika hiyo sehemu yakiisha iva yavuruge na kisha yachanganye pamoja na vegetable na kisha tia chumvi kidogo sana. Baada ya hapo malizia kwa kutia wali na soy source kisha koroga vizuri mpaka mchanganyiko wako wote  uchanganyike vizuri (hakikisha wali unapata
 moto na vegetable haziivi sana) . Na baada ya hapo chakula chako kitakuwa tayari.

Saturday, 5 March 2011

Mapishi ya Kuku wa kukaanga



Mahitaji
Miguu ya kuku (chicken legs) 10
Kitunguu swaum na tangawizi (ginger & garlic paste) 1 kijiko cha chakula
Limao (lemon) 1
Pilipili iliyosagwa (ground scotch bonnet) 1/2
Giligilani iliyokatwakatwa (chopped coriander) kiasi
Chumvi (salt) kiasi
Mafuta ya kukaangia (veg oil)

Matayarisho
Safisha kuku kisha mtie kwenye sufuria na viungo vyote (kasoro mafuta na giligilani) kisha mchemshe mpaka aive na umkaushe supu yote. Baada ya hapo mkaange katika mafuta mpaka awe wa brown kisha mtoe na uweke katika kitchen towel ili kuchuja mafuta. Baada ya hapo weka katika sahani na umwagie giligilani kwa juu. Na hapo kuku wako atakuwa tayari kwa kuliwa.

Thursday, 3 March 2011

Mapishi ya Half cake (Keki)


Mahitaji
Unga wa ngano (self risen flour) kikombe 1na 1/2
Sukari (sugar) 1/4 kikombe
Barking powder 1/2 kijiko cha chai
Magadi soda (bicarbonate soda) 1 kijiko cha chai
Mafuta 2 vijiko vya chai
Mafuta ya kukaangia
Maji ya uvuguvugu kiasi

Matayarisho
Changanya unga na vitu vyote (kasoro mafuta ya kuchomea) kisha ukande (hakikisha unakuwa mgumu) Baada ya hapo sukuma na ukate shape uipendayo (hakikisha unakata vipande vinene kiasi na sio kama mandazi) Baada ya hapo ziweke sehemu yenye joto na uache ziumuke. Zikisha umuka zikaange katika moto mdogo ili ziive mpaka ndani. Zikisha iva zitoe na uziweke katika kitchen towel ili zichuje mafuta. Ziache zipoe na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.