Thursday 18 August 2011

Mkate wa mayai


Mahitaji
Slice za mkate 6
Mayai 3
Chumvi
Olive oil

Matayarisho
Vunja mayai yote katika sahani kisha tia chumvi kidogo sana na uyapige mpaka chumvi ichanganyike. Kisha chukua frying pan na utie vimafuta kidogo na uweke jikoni. Mafuta yakishapata moto kiasi,chovya slice za mkate katika hayo mayai na  uzipike pande zote zikishaiva zitoe na uziweke katika kitchen towel ili kukausha mafuta.Na baada ya hapo mikate yako itakuwa tayari kwa kuliwa na chai.

2 comments:

  1. asante sana,je km sina olive oil naweza kutumia mafuta mengine ya kupikia?

    ReplyDelete
  2. Asante. Ndiyo unaweza kutumia mafuta yoyote uyapendayo iwe vegetable oil, sunflower oil au yoyote yale.Mi huwa napenda kutumia olive oil kwasababu wataalam wanasema mazuri kwa afya kuliko hayo mengine.

    ReplyDelete