Friday 15 July 2011

Mapishi ya Shami kebab


Mahitaji
Nyama ya ng'ombe (steak)1/4 kilo
Dengu kavu 1/2 kikombe
Giligilani ya unga 1/2 kijiko cha chai
Binzari nyembamba ya unga 1/4 kijiko cha chai
Swaum/tangawizi kijiko 1 kikubwa cha chakula
Chumvi kiasi
Curry powder 1 kijiko cha chai
Pilipili kali  1/2
Yai 1
Mafuta ya kukaangia
Kitunguu maji kilichokatwakatwa
Limao 1/2

Matayarisho
Chemsha nyama na limao na chumvi mpaka iwe laini. Na pia chemsha dengu nazo mpaka ziwe laini. Baada ya hapo tia nyama,dengu na spice zote ktk blender (kasoro vitunguu,majani ya giligilani, yai) Visage mpaka viwe laini kisha tia ktk bakuli. Baada ya hapo malizia kwa kutia vitu vilivyobaki.Changanya vizuri kisha tengeneza kebab zako shape ya round (kama uonavyo kwenye picha) kisha zikaange ktk mafuta ya kiasi. Baada ya hapo zitakapoiva zitakuwa tayari kwa kuliwa.Unaweza kuzisev na salad uipendayo.

No comments:

Post a Comment