Thursday 14 April 2011

Mapishi ya Maini ya ng'ombe


Mahitaji
Maini (Cow liver) 1/4 kilo
Vitunguu (chopped onion) 2
Nyanya (chopped  tomato) 1
Kitunguu swaum/tangawizi (ginger /garlic paste) 1 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia
Chumvi
Coriander
Curry powder 1 kijiko cha chai
Limao (lemon) 1/4
Pilipili (scotch bonnet ) 1

Matayarisho
Safisha maini na ukate vipande vidogovidogo na uweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu kidogo(visiwe vya brown) kisha tia ginger/ garlic paste,carry powder kaanga kidogo kisha tia nyanya. Kaanga nyanya mpaka zitoe mafuta kisha tia chumvi, pilipili na vimaji kidogo. Acha vichemke kidogo kisha tia maini na uyapike mpaka yaive. Malizia kwa kukamulia limao na kutia coriander kisha ipua na hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa.

3 comments:

  1. Mmmh..., napenda sana maini. Mimi huwa kwanza kabla ya kuyakata natoa ile ngozi laini ili yasiwe magumu.

    ReplyDelete
  2. Mh hilo ni wazo zuri. Ila mimi mara nyingi huwaga sitoi hiyo ngozi.Napikaga nayo hivyohivyo ila kuhakikisha maini hayawi magumu nakata vipande vidogovidogo sana na kisha huwa siyapiki kwa muda mrefu.

    ReplyDelete
  3. MAINI HUWA YANA WADUDU WANAOSABABISHA MAGONJWA,KWANINI WATU HAWAPENDI KUPIKA SANA MPAKA YAIVE? NI HATARI

    ReplyDelete