Saturday 12 February 2011

Mapishi ya Tandoori chicken (kuku)


Mahitaji

  • Kuku mzima 1 ( A whole chicken)(mimi huwa natumia baby chiken)
  • Kitunguu swaum/tangawizi (garlic & ginger paste) 1 kijiko cha chai
  • Maziwa ya mgando (plain yogurt )1 kikombe cha chai
  • Curry powder 1/2 kijiko cha chai
  • Garam masala 1/2 kijiko cha chai
  • Coriander powder 1/2 kijiko cha chai
  • Cumin powder 1/2 kijiko cha chai
  • Chilli powder 1/2 kijiko cha chai
  • Limao (lemon)1/2
  • Chumvi (salt ) kiasi
  • Rangi ya chakula nyekundu (food colour) few drops
  • Mafuta ya kupikia (vegetable oil) vijiko 2 vya chakula
Matayarisho
Katakata kuku katika vipande vya kawaida kisha umuoshe na umkaushe maji kwa kutumia kitchen towel. Baada ya hapo muweke katika bakuli kubwa na uanze kutia limao na spice zote kasoro mafuta, yogurt na rangi ya chakula. Changanya spice na kuku mpaka vikolee vizuri. Baada ya hapo changanya yogurt na rangi ya chakula pembeni na kisha umwagie katika kuku na uchanganye tena vizuri. Baada ya hapo malizia kwa kutia mafuta na uchanganye vizuri kisha funika na uweke katika friji kwa muda wa masaa 3 ili kuku aingie viungo.
Baada ya hapo muoke kuku wako katika oven kwa muda wa nusu saa katika moto wa 200°C.Baada ya hapo kuku wako atakuwa tayari kwa kuliwa.

Mtanisamehe picha imekaa upande maana niliipiga vibaya


2 comments:

  1. Mmmmh... it looks delicious and simple to cook. I love Chicken Tandoori 'yummy' na nilikuwa sijui kuipika, Asante sana kwa recipe

    ReplyDelete
  2. Unakaribishwa Nancy. mimi pia huwa napenda sana mapishi simple unakuwa hupotezi muda sana jikoni.

    ReplyDelete