Monday 28 February 2011

Mapishi ya Aloo vada


Mahitaji

  • Viazi ulaya vya wastani (Potato) 5
  • Kitunguu maji (onion) 1/2
  • Kitunguu swaum na tangawizi( ginger and garlic paste) 1 kijiko cha chai
  • Unga wa dengu (garam flour) 1/2 kikombe cha chai
  • Giligilani iliyokatwakatwa (fresh chopped coriander) kiasi
  • Curry powder 1/2 kijiko cha chai
  • Turmaric 1/4 kijiko cha cha chai
  • Chilli powder 1/4 ya kijiko cha chai
  • Chumvi (salt) kiasi
  • Mafuta ya kukaangia (veg oil)
Matayarisho
Chemsha viazi mpaka vilainike kisha viponde na uviweke pembeni. Baada ya hapo katakata  kitunguu maji vipande vidogovidogo na uvitie katika viazi,kisha malizia kwa kutia vitu vyote vilivyobaki(kasoro mafuta ya kukaangia).Baada ya hapo changanya vizuri kisha utengeneze shape uipendayo (inaweza kuwa maduara  au ring) Baada ya hapo zikaange katika moto wa wastani mpaka ziive. Na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

No comments:

Post a Comment