Monday 6 September 2010

Mapishi ya Potato wedges na samaki wa kuoka



Mahitaji

  • Viazi ulaya (baking potato 5 vya wastani)
  • Parprika 1 kijiko cha chai
  • Pilipili mtama ilyosagwa (ground black pepper 1 kijiko cha chai
  • Kitunguu swaum cha unga (garlic powder 1 kijiko cha chai)
  • Chumvi (salt)
  • Mafuta (vegetable oil)
  • Marination za samaki (angalia kwenye recipe ya samaki ya nyuma)
Matayarisho
Osha viazi na maganda yake kisha vikaushe na uvikate vipande vya wastani. Kwa kila kiazi toa vipande 6. Kisha vitie kwenye bakuli na utie parpika, pilipili mtama ya unga, kitunguu swaum cha unga, chumvi na mafuta kama vijiko 2 vya chakula. Changanya pamoja na kisha uvibake katika oven kwa muda wa dakika 25. Hakikisha vinakuwa rangi ya brown. Vikisha iva vitoe.
Wamarinate samaki, na uwaoke kisha wasevu na potato wedges tayari kwa kuliwa
(Jinsi ya kupika samaki, angalia katika recipe za nyuma)

No comments:

Post a Comment