Sunday 12 September 2010

Jinsi ya Kupika Kalmati



Mahitaji

  • Unga wa ngano (self risen flour 2 vikombe vya chai)
  • Hamira (yeast kijiko 1 cha chai)
  • Sukari (sugar 2 vikombe vya chai)
  • Hiliki (cardamon 1/4 ya kijiko cha chai)
  • Maji kikombe1 na 1/2
  • Mafuta
Matayarisho
Changanya unga, hamira, maji na mafuta kijiko 1. Koroga vizuri mpaka upate uji mzito usiokuwa na madoge Baada ya hapo uache uumuke kisha zichome kalmati katika moto wa wastani. Baada ya hapo tia sukari, hiliki na maji 1/2 kikombe katika sufuria na ichemshe uku unakoroga mpaka iwe tayari.(ukitaka kujua kama iko tayari chovya mwiko kisha gusa na vidole utaona iko kama nta au gundi) Baada ya hapo tia kalmati na uzichange pamoja mpaka zikolee kisha zitoe na uziache mpaka zipoe tayari kwa kuliwa.

3 comments:

  1. Maelezo haya hayajatulia. Tafadhali unaweza akiki?

    ReplyDelete
  2. Hebu nomba unieleweshe unamaana gani unaposema uszichome. Umeniacha njiani. Naomba unielezee vizuri. Ninahamu ya kuzipika sana..TX..

    ReplyDelete
  3. Kuzichoma maana yake ni kuzikaanga katika mafuta ya moto.

    ReplyDelete