Wednesday 27 April 2011

Jinsi ya kupika Fish cakes


Mahitaji
Fish fillet (steki ya samaki isiyokuwa na mifupa) kipande 1 kikubwa
Viazi (potato) 6 vya wastani
Kitunguu (onion) 1 kikubwa
Tangawizi na swaum (garlic and ginger paste) 1 kijiko cha cha chai
Breadcrumbs kiasi
Mayai (eggs) 2
Limao (lemon) 1/2
Chumvi (salt) kiasi
Pilipili (scotch bonnet chilli) 1/4
Curry powder 1/2 cha chai
Coriander powder 1/4 kijiko cha chai
Turmaric 1/4 kijiko cha chai
Fresh chopped coriander kiasi.
Mafuta ya kukaangia

 Matayarisho
Chemsha viazi na chumvi kidogo kisha viponde na uviweke pembeni vipoe.Katakata samaki vipande kisha mtie kwenye sufuria pamoja na tangawizi, swaum, limao na chumvi. Mchemshe kidogo(hakikisha maji yote yanakauka) kisha mponde na uma (folk) baada ya hapo tia spice zote,pilipili na vitunguu vilivyokatwa vidogovidogo na uvipike pamoja na samaki kwa muda wa dk 3. Baada ya hapo tia coriander na kamulia limao kisha viweke pembeni. Baada ya hapo changanya viazi pamoja na mchanganyiko wa samaki kisha tengeneza maduara ya wastani. Baada ya hapo piga mayai ktk bakuli na chumvi kidogo.Bandika jikoni mafuta  ya kukaangia ktk fry pan yawe kidogo tu (shallow fry) yakisha pata moto kiasi chukua madonge yako kisha yachovye ktk mayai na umalizie ktk breadcrumbs kisha zikaange ktk mafuta. Baada ya hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa

Sunday 24 April 2011

Egusi


Mahitaji
Spinach 1/2 packet au Mafungu 2
Egusi (ground pumpkin seeds) 4 vijiko vya chakula
Dagaa 1/2 kikombe
Nyanya ya kopo (tin tomato) 1/2
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Curry powder 1/4 kijiko cha chai
Kitunguu (onion) 1
Pilipili (scotch bonnet chilli) 1/2
Kitunguu swaum na tangawizi (garlic and ginger paste) 1 kijiko cha chai
Maggi cubes 1
Lemon 1/4
Chumvi (salt)
Mafuta ya kupikia

Matayarisho
Osha,katakata spinach na zikaushe maji kisha ziweke pembeni. Saga pamoja nyanya, kitunguu, pilipili, garlic na ginger kisha tia kwenye sufuria na uvipike mpaka maji yote yakauke.Baada ya hapo tia dagaa,curry powder na mafuta kiasi, Zikaange pamoja kwa muda wa dakika tano na ukamulie limao. Baada ya hapo katika bakuli tia egusi na maji kiasi kisha ikoroge mpaka madonge yote yatoke na uitie kwenye mchanganyiko wako kisha tia maggi cube na maji kidogo na upike kwa muda wa dakika 30 pia mpaka maji yakauke na upate paste nzito.Baada ya hapo Tia spinach na uzipike mpaka ziive, kisha ipua na mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Inapendeza zaidi ukilia na ugali malaiiiini.

Note:
Ukisha tia egusi unatakiwa upunguze moto kwa maana moto ukiwa mkubwa haikawii kushika na kuungua chini. Pia usitie chumvi baada ya kuweka maggi cube kwa maana zina chumvi.kwa hiyo unatakiwa kuonja kwanza kabla ya kuongeza chumvi.



Wednesday 20 April 2011

Chips (homemade)


Mahitaji
Viazi (potato) 1/2 kilo
Mafuta ya kukaangia (veg oil)
Chumvi

Matayarisho
Menya viazi kisha vioshe na vikaushe maji yote kwa kutumia kitchen towel.Baada ya hapo katakata katika shape ya chips uzipendazo either nyembamba au nene kisha zikaushe tena maji na uzitie chumvi. Baada ya kuzitia chumvi tu zitie kwenye mafuta ya kukaangia straightaway (hakikisha mafuta yasiwe ya moto sana kwani utazibabua) Zipike upande mmoja ukiiva geuza upande wa pili. Baada ya hapo endelea kuzipika uku ukiwa unazigeuzageuza mpaka kwa nje ziwe light brown na crisps.Baada ya hapo zitoe na uziweke kwenye kitchen towel ili zichuje mafuta na zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Sunday 17 April 2011

Mapishi ya Chapati za maji za vitunguu


Mahitaji
Unga wa ngano (plain flour) 1/4
Kitunguu kikubwa (chopped/slice onion) 1
Yai (egg) 1
Chumvi (salt)
Mafuta (cooking oil)

Matayarisho
Tia unga, chumvi na maji kiasi katika bakuli kisha koroga mpaka madonge yote yaondoke. Baada ya hapo tia yai na vitunguu kisha koroga tena mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. baada ya hapo choma chapati zako kama kawaida (jinsi ya kuchoma unaweza kuangalia kwenye recipe yangu ya chapati za maji katika older posts) na baada ya hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Thursday 14 April 2011

Mapishi ya Maini ya ng'ombe


Mahitaji
Maini (Cow liver) 1/4 kilo
Vitunguu (chopped onion) 2
Nyanya (chopped  tomato) 1
Kitunguu swaum/tangawizi (ginger /garlic paste) 1 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia
Chumvi
Coriander
Curry powder 1 kijiko cha chai
Limao (lemon) 1/4
Pilipili (scotch bonnet ) 1

Matayarisho
Safisha maini na ukate vipande vidogovidogo na uweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu kidogo(visiwe vya brown) kisha tia ginger/ garlic paste,carry powder kaanga kidogo kisha tia nyanya. Kaanga nyanya mpaka zitoe mafuta kisha tia chumvi, pilipili na vimaji kidogo. Acha vichemke kidogo kisha tia maini na uyapike mpaka yaive. Malizia kwa kukamulia limao na kutia coriander kisha ipua na hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa.

Sunday 10 April 2011

Mapishi ya Mlenda wa bamia na nyanya chungu


Mahitaji
Bamia (okra) 20
Nyanya chungu (garden eggs) 5
Magadi soda (Bicabonate soda) 1/4 ya kijiko cha chai
Nyanya (fresh tomato) 1
Chumvi (salt) kidogo
Pilipili 1/4

Matayarisho
Osha bamia, nyanya chungu na nyanya kisha vikatekate katika vipande vidogovidogo. Baada ya hapo vitie kwenye sufuria na vitu vyote vilivyobakia na kisha tia  maji kidogo.Chemsha mpaka bamia na nyanya chungu ziive na vimaji vibakie kidogo sana. Baada ya hapo ziponde na mwiko kidogo kisha zikoroge na uipue na mlenda utakuwa tayari kwa kuliwa na ugali.

Thursday 7 April 2011

Mapishi ya Wali wakukaanga


Mahitaji
Mchele (Basmati rice) 1 kilo
Vitunguu (chopped onion) 2 vikubwa
Garlic powder 1/2 kijiko cha chai
Njegere (peas) 1 kikombe
Turmaric 1/2 kijiko cha chai
Coriander powder 1/2 kijiko cha chai
Cumin seeds 1/2 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia 2 vijiko vya chakula
Chumvi kiasi

Matayarisho
Osha kisha loweka mchele kwa muda wa dakika 5 na kisha uchuje maji na uweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown na kisha tia spices zote.Zikaange kwa muda wa dakika 3 kisha tia mchele na uchanganye vizuri na spice.Ukaange mchele pamoja na spice uku ukiwa unageuzageuza kwa muda wa dakika 5. Baada ya hapo tia maji ya moto(kiasi ya kuivisha wali) na chumvi kisha ufunike. Upike mpaka uive kisha malizia kwa kutia njegere na uchanganye vizuri baada ya dakika 2 uipue utakuwa tayari kwa kuliwa.Unaweza kuula kwa mboga yoyote uipendayo

Monday 4 April 2011

Broccoli soup


Mahitaji
Broccoli Kichane 1
Viazi (potato) 2 vya wastani
Supu (chicken or vegetable broth) 2 vikombe
Kitunguu (onion) 1 kikubwa
Mafuta ya kupikia 1 kijiko cha chakula
Chumvi (salt) kiasi
Pilipili 1/4
Limao 1/4

Matayarisho
Katakata broccoli, viazi na kitunguu katika vipande vya wastani kisha viweke katika sufuria ya kuchemshia na utie maji kidogo na chumvi. Chemsha mpaka viazi na broccoli viive kisha tia supu, pilipili, mafuta na ukamulie limao baada ya hapo chemsha tena kwa dakika 5 na baada ya hapo isage na itakuwa tayari kwa kuseviwa

Friday 1 April 2011

Mapishi ya Sponge keki


Kwa walioniomba recipe ya sponge cake hiyo ni kwa ajili yenu.

Mahitaji
Unga wa ngano (self risen flour) 100g
Sukari (sugar) 100g
Siagi isiyokuwa na chumvi (unsalted butter) 100g
Mayai (eggs) 2
Vanila 1 kijiko cha chai
Chumvi pinch
Warm water 3 vijiko vya chakula

Matayarisho
Kwanza washa oven moto wa 200 C. Baada ya hapo saga butter na sukari mpaka viwe laini kisha tia mayai na uendelee kusaga mpaka vichanganyike vizuri kisha tia unga, vanila, chumvi na na maji na usage mpaka upate uji usiokuwa mzito sana au mwepesi sana. Baada ya hapo utie kwenye baking tin na u bake kwa muda wa dakika 25 na mpaka cake yako iive yani juu na chini iwe ya brown na ukidumbukiza kijiti katikati kinatoka kikiwa clean. Baada ya hapo itoe kwenye tin na uiache ipoe. Ikisha poa itakuwa tayari kwa kuliwa.